Na Mwaandishi wetu Mtwara

TAASISI ya Utafiti wa kilimo nchini (TARI) Naliendele kwa kushirikiana na Bodi ya korosho nchini (CBT) wameanzisha mkakati wa kuwapa wakulima elimu juu ya ulimaji bora wa zao hilo ili kuongeza uzalishaji kutoka tani 300,000 mpaka kufikia 1,000,000 kwa mwaka.

Mtafiti upande wa wadudu hawaribifu na magonjwa ya mikorosho kutoa TARI Naliendele Dadili, Majune amesema elimu ya kilimo cha korohosho haijafikia wakulima wengi nchini kuweza kupata mbinu mpya na za kisasa katika ulimaji bora na wa tija kwa zao hilo.

“Tumeamua tuwe na mafunzo haya ili wakulima waweze kuhakikisha kwamba wanazalisha korosho kwa wingi, kwa ajili ya kuinua taifa na familia zao,” amesema Majune

Amesema kuwa yamekuwepo matatizo mengi kwa wakulima jinsi ya kutunza mikorosho wakiwemo wadudu kwenye mikorosho ambayo yanasababisha uharibu wa za hilo kwa asilia hamsini.

“Tukienda kwenye upande wa wadudu waharibifu wa mikorosho , wanasababisha hasara kubwa kwenye mkorosho, zaidi ya asilimia 50 ya zao hilo shambani huharibiwa kama wasipodhibitiwa,” amesema.

Kwa upande wa magonjwa, Majune amesema magonjwa husababisha hasara ya zaidi ya asilimia 70 mpak 100 ya mazao yote shambani na usipodhibitiwa mkulima anaweza asipate chochote.

“Lakini kupitia mkakati huo, wataalamu tutawafundisha wakulima na mabwana shamba, elimu kuhakikisha kwamba tatizo la wadudu waharibifu linaisha na kupata korosho bora na kuongeza tija na wapate mavuno ya kutosha na kipato cha kuendesha familia zao,” amesema.

Amesema kuna maeneo wakulima ‘wanafeli’ kwa kutokufuata maelekeza wanayopewa na mabwana shamba, hivyo kusababisha hasara kubwa katika ukuaji wa zao la korosho

“Kwa hiyo tunazidi kuwasisitiza kwamba elimu wanayoipta waifanyie kazi kwa kufuatilia kwa sababu wakulima wengi wanapenda kufuatilia vitu nje, wawe na elimu kwamba ni kiwatilifu gani kinafaa na viwe vilivyopitishwa na naliendele,” amesema.

Majune aliomba serikali kuongeza maafisa kilimo ili waweze kuwasaidia kutoa elimu na kuwasimimia wakulima kuzingatia kilimo cha tija na kuhakikisha ubora na mavuno mengi ya korosho nchini.

Kwa upande mwingine, wakulima mkoani hapa wameonyesha kufurahishwa na kitendo cha TARI Naliendele na Bodi ya korosho, kuanzisha mkakati wa kuwapa elimu juu ya ulimaji bora wa zao la korosho.

Wakizungumza mara baada ya kushiriki katika mafunzo ya vitendo katika shamba la serikali Magereza mkoani hapa, wakulima hao wamesema mafunzo hayo ni muhim sana na yatawasaidia katika kujua na kufuata kanuni bora cha kilimo cha zao hilo.

“Mafunzo ni mazuri sana na endapo serikali itafanya mara kwa mara, nafikiri wakulima wa hali ya chini tutaelimika na kufaidika sana kwa kupanda na kupata korosho iliyo boro, wengine sisi tuna mashamba ambayo kwa kweli tulivyo yapandapanda hayaeleweki,” amesema Mohammed Bakari Mkulima wa korosho wilaya ya Mtwara.

Bakari ameishukuru wahusika kwa hatua hiyo ya kutoa mafunzo na kusema kwamba ingekuwa bora Zaidi mafunzo hayo kutolewa mara kwa mara ili kuwafikia wakulima wa chini kabisa .

“Binafsi sijawai kupata mafunzo kama haya, hii ndio mara yangu ya kwanza na nimefaidika kwa kiasi na nikiondoka hapa naenda kubadilisha na kuanza kulima kwa kisasa n ahata kubadilisha miti ya mikorosho ya zamani na kupanda mipya ili kuongeza mavuno,” amesema

Adam Mathew mkulima kutoka Mikindani amesema mafunzo hayo yanawapa uelewa kujua nini kifanya wakati wa kuandaa shamba na kupanda zao la korosho ili liweze kustawi na kuongeza mavuno.

“Mafunzo haya wanatupa fursa ya kuangalia mbali katika kilimo chetu na kuwa waangalifu kwa sababu kilimo cha sasa hivi sio kama kilimo cha zamani ambapo babu zetu waliamka na kwenda shambani na kulima na kusubiri kuvuna tu,” amese na kuongeza “Lakini kilimo cha sasa kina mambo mengi ambayo yanahitaji mkulima awe na elimu jinsi ya kutumia madawa, kupanga mbegu na kuandaa shamba.”

Mathew ameiomba serikali kuweka mfumo wa ambao utahakikisha wakulima wanapata mafunzo ya namna hiyo kabla ya msimu wa mavuno kuanza ili kuwasaidia wakulima kuandaa na kuzingatia kanuni bora za kulima zao la korosho.

Baadhi ya Wakulima wakiwa kwenye shamba la mikorosho mfano la Serikali, Magereza wakipata mafunzo ya vitendo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...