Mtendaji Mkuu wa TGT, Anna Domick (kulia) akimkabidh, Bi.Esther Hanai mashine ya nguo kwa ajili ya shughuli za kijasiriamali, katikati ni Meneja miradi wa TGT, George Mwafula.

Na mwandishi wetu, Michuzi TV

KATIKA harakati za kukuza vipato vya wajasiriamali akinamama nchini taasisi ya Tanzania Groth Trust (TGT) kupitia programu yake ya 'MKubwa' imewawezesha mashine za viwanda vidovidogo akinamama waliojiunga na programu hiyo ili waweze kufanya shughuli za uzalishaji na kujipatia vipato vitakavyowasaidia kukuza familia zao.

Hayo yamesema na Mtendaji wa mkuu wa taasisi hiyo, Anna Dominick wakati  akitoa msaada huo kwa akinamama ili waweze kuutumia kuzalisha mali na kupata vipato vya kukidhi mahitaji yao pamoja na familia zao.

“Tumewawezesha vitendea kazi, hivi ni viwanda vidogovidogo katika sekta ya nguo, usindikaji na kazi za mikono” vitendea kazi hivi tumewapatia kulingana na mafunzo  ya ujasiriamali mliyoyapata," amesema.

Amesema kuwa vitendea kazi hivyo ni mashine za kusindika mazao, mashine za ushonaji nguo, na vifaa vya saluni.

Aidha amesema kuwa taasisi hiyo inatoa mafunzo ya ujasiriamali kwa akinamama na kuwaunganisha ili wapate mikopo kutoka mfuko wa taasisi hiyo pamoja na taasisi mbalimbali za kifedha zikiwemo taasisi za Serikali.

Bi. Dominick amesema kuwa, lengo la kufanya hivyo ni kuwawezesha ili waweze kuongeza uzalishaji zaidi, kwa ubora na waweze kuyafikia masoko ya ndani na nje ya nchi kwa kuzingatia na  kulinda nidhamu ya shughuli zao.

Mmoja ya wanufaika wa vitendea kazi hivyo,  Jonecia John  amesema kuwa alijiunga na programu ya 'Mkubwa' mwaka 2010 na alipata mafunzo na kushiriki maonyesho mbalimbali.

“Nimewezeshwa na sasa mimi ni mkufunzi , na nawahitaji akinamama wanaposikia fursa kama hizi wasidharau,” amesema.

Pia Mwanahawa  Saleh amesema, tangu ajiunge na programu ya 'Mkubwa' kupitia TGT na amepata mafanikio makubwa na  kupata msaada wa kitendea kazi na mtaji utatatua changamoto mbalimbali. 

“Awali sikujua chochote kwa sasa naweza kusindika mazao, kutengeneza mikoba na viatu kwa kuweka nakshi ya shanga, na nahitaji kukuza mradi wangu ili niwe mfanyabiashara mkubwa" amesema Mwanahawa.


 


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...