Baadhi ya wazee 

Baadhi ya wanachama wa chama cha Askari wastaafu wa Vita Kuu ya pili ya dunia vya mwaka 1939 hadi 1945 ambao ni watoto na wajukuu wa wazee waliowahi pigana vita vya pili vya dunia.
Afisa Tawala TLC, Charles Lubala akizungumza wakati wa mkutano mkuu wa Chama cha Askari wastaafu wa Vita Kuu ya pili ya dunia vya mwaka 1939 hadi 1945 uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Mjumbe wa Task Force, TLC, Kapten Mstaafu Mohamed Ligora akizungumza kabla ya kufanya uchaguzi waviongozi mbalimbali jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya Medali zwalizowahi kutunukiwa mara baada ya vita ya pili ya dunia kuisha.

Na Avila Kakingo, Globu ya Jamii
CHAMA cha Askari wastaafu wa Vita Kuu ya pili ya dunia vya mwaka 1939 hadi 1945 kinayojumuisha watoto na wajukuu wao (Tanzania Legion and Clubs) wafanya uchaguzi wa viongozi ambao ni kwa mujibu wa katiba yao unaofanyika kila baada ya miaka mitatu.

Uchaguzi wa mwaka huu 2020 ni uchaguzi wa saba kati ya chaguzi ambazo zimeshawahi kufanyika mikoa tofauti na kwa mwaka huu uchaguzi huo umefanyika jijini Dar es Salaam.

Walioshinda katika uchaguzi huo kwa nafasi ya Mwenyekiti wa chama cha TLC ni Baruti Siriri ambaye ameshinda kwa kura 32 kati ya kura 59, Makamu Mwenyekiti ni Hamis Yazid Kwizombe ameshinda kwa kura 19 kati ya kura 59 ambapo wagombea wengine wawili walifungana kwa kura 17.

Kwa nafasi ya Katibu Mkuu wa Chama hicho ameshinda Charles Lubala ambaye alipita bila kupingwa akiwa sambamba na Mwekahazina wa chama chicho, Agnes Kehuro ambaye pia amepita bila kupingwa.

Wakati huo huo wamefanya uchaguzi wa kamati kuu, bodi ya wadhamini na kamati tendaji ya chama cha Askari wastaafu wa Vita Kuu ya pili ya dunia vya mwaka 1939 hadi 1945.

Kwa upande wa bodi ya wadhamini waliopata nafasi ni Pius Chacha, Shabani Siriri, Batazar Wambura, Kepteni, Athuman Ligora na Nelson Machimu.

Kwa mujibu wa katiba ya chama hicho ameunda kamanti tendaji ya wajumbe sita(6) pamoja na kamati ya halmashauri kuu ya watu 16.

Licha ya kupata viongozi wa chama cha Askari wastaafu wa Vita Kuu ya pili ya dunia (TLC) kinachojumuisha watoto na wajukuu wao wameiomba serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutambuliwa na Wizara ya habari, utamaduni na Michezo pamoja kitengo cha mambo ya kale katika historia ya ukombozi wanchi hii kwa wale waliohai mpaka sasa.

Kwa upande waliotangulia mbele ya haki (Waliofariki dunia) wameomba makaburi yao yatambuliwe kwa kujengewa makaburi ya kudumu ili iwe alama itakayodumu kwa vizazi vya leo na vizazi vijavyo.

Akizungumza wakati akisoma lisala ya chama cha TLC, Afisa Tawala, Charles Lubala amesema kuwa kunabaadhi ya maafisa waandamizi wa serikali wamekuwa kikwazo kinachokwamisha kwa makusudi ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo endelevu ya kiuchumi na kijamii ya TLC yanayokusudiwa kufanywa kwa maslahi ya wanachama.

Hata hivyo wameomba Serikali kutowang'ang'ania mavetenari wa chama hicho kuendelea kuongoza chama hicho huku wakiwa na umri mkubwa na huku wakisumbuliwa na maradhi mbalimbali ambapo inawapa wakati mgumu kuongoza chama hicho hivyo kusababisha kudorora kwa baadhi ya kazi za kama hicho.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...