Mgombea Urais kwa Tiketi ya Chama cha Mapinduzi CCM Rais Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akicheza juu ya Gari yake mara baada ya kuzungumza na wananchi wa Dodoma mjini wakati akitokea mkoani Tabora kwenye mikutano ya Kampeni ya CCM jana Septemba 22, 2020



Na Said Mwishehe-Michuzi TV


MTANZANIA mwenzangu naomba nikumbushe tu kampeni za Uchaguzi Mkuu mwaka 2020 zinaendelea kwa wagombea wa vyama vyote kupita kwa Watanzania kuomba kura.


Ndio wamekuwa wakipita kuomba kura ambapo wanatumia nafasi hiyo kueleza yale ambayo watafanya katika nchi yetu iwapo watapata ridhaa ya kuongoza nchi. Wanapita, wanajieleza na tunawasikia.


Kazi itabaki kwetu kufanya maamuzi na sio maamuzi tu bali ni maamuzi sahihi.


Kwa nafasi ya urais kwa mujibu wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) waliopitishwa kugombea wapo wagombea urais 15. Hata yule mgombea mwenye sera za kwamba akichagulikuwa kuwa Rais wa Tanzania watu watakuwa wanakula ubwabwa naye yumo. Ndivyo demokrasia ya nchi yetu ilivyo na kazi itabaki kwetu kuamua.


Hata yule ambaye anayesema kwamba wakoloni walijenga reli Kaulia mpaka Mpanda imekufa naye yumo, hajui hata kama reli hiyo ipo na inafanya kazi vizuri. 


Inasikitisha sana unapokuwa na mgombea urais ambaye anatumia kampeni za uchaguzi mkuu kuongopa.Na Watanzania wana akili sana kwani wanamsikiliza kisha wanabaki wanamcheka tu.


Wakati kampeni zikiendelea na wagombea tukiendelea kuwasikiliza, naomba nikiri kati ya wagombea wote 15 ambao wamepita kuomba kura hadi sasa kwa Watanzania mwenye sifa zote za kuwa Rais wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni mmoja tu, ni Dk.John Pombe Joseph Magufuli.


Ana sifa zote za kuwa Rais wetu , ana kila sababu za kuchaguliwa kuwa Rais ifikapo Oktoba 28 mwaka huu. Ndio anastahili kwasababu anayosema Watanzania wanamuelewa, anayotenda Watazania wanaona. Ni Dk.Magufuli ambaye kwenye kampeni zake anaeleza nchi ilikotoka, ilipo na inakokwenda.


Dk.Magufuli huwezi kumfananisha na mgombea mwingine yoyote , ukiondoa sifa ya msingi kwamba wote ni wa Watanzania lakini yeye amekwenda mbele zaidi sio mtanzania tu bali ni Mtanzania mzalendo, mtanzania mnyenyekevu, mtanzania mwenye kujua mahitaji ya watanzania. ni mtanzania anayejua kujali na kupenda watu wake, ni mtanzania ambaye hayuko tayari kuona rasilimali za nchi yake zinachezewa.


Ni Dk.Magufuli ambaye kwenye kampeni zake anazungumzia zaidi maendeleo ya nchi yake, amekuwa akizungumzia jinsi gani Ilani ya Uchaguzi Mkuu ya CCM yenye kurasa 303 ilivyosheheni mambo makubwa kwa ajili ya Taifa hili.Ni Dk.Magufuli anayezungumzia kuwaunganisha Watanzania na kuwahimiza kuendelea kufaya kazi kwa bidii.


Sawa kwa mujibu wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi(NEC) wagombea urais wako 15 lakini ukweli utabaki pale pale mwenye sifa ni moja tu.


Watanzania wanamuelewa zaidi Dk.John Magufuli, katika miaka mitano ya uongozi wake amefanya mambo makubwa.  Sote ni mashahidi, sote tumeona, sote tunamuelewa.Ndio maana wengi wetu tunasubiri Oktoba 28 tu tukafanye maamuzi.


Kwa akili ya kawaida hapa kuna Dk.Magufuli kule kuna hao akina wenzangu na mimi, kura yako inakwenda wapi? Itakwenda kwa Dk.Magufuli. Watanzania wengi wanasema katika uchaguzi mkuu mwaka huu ni mitano tena kwa JPM.Ndio wanavyosema, baki na ubishi wako kama utakusaidia.


Dk.Magufuli ameingia kwenye kampeni tayari Watanzania wakiwa wanajua amefanya nini katika kipindi cha miaka mitano ambayo ameiongoza nchi.


Na sio kuiongoza tu bali kuiongoza katika mfumo ambao kila Mtanzania sasa amebaki na tumaini la kwamba sasa tunaye kiongozi.Tuna kiongozi mwenye mapenzi mema na nchi yake.Ahsante Mungu kwa zawadi hii nzuri ya kuwa na Dk.John Magufuli.


Ahsante Mungu kwa sababu unajua Watanzania tunamuhitaji zaidi Dk.Magufuli na katika uchaguzi Mkuu wa Oktoba 28 tutathibitisha hilo kwa kumpa kura nyingi. Watanzania wameshaamua hao wengine wacha wazunguke tu huko mtaani. 


Kwanza hawana jipya, hawana la maana kazi yao ni kuzusha , kupotosha na kuficha ukweli.Nawaaambia wala hawana nafasi.

Dk.Magufuli amefanya makubwa sana katika kipindi cha miaka mitano.Sitaki kuzungumzia kuhusu janga la Corona ambalo ametuvusha na leo tunadunda tu mtaani. Alisema tumtangulize Mungu na tukafanya hivyo leo mambo yetu safi kabisa.


Katika kuleta maendeleo Dk.Magufuli ameifanya kazi hiyo vizuri sana. Ameifanya kwa uaminifu mkubwa, ameifanya bila kuchoka, ameifanya akitanguliza uzalendo kwa nchi yake.Kabla ya kampeni kuanza tayari Dk.Magufuli anao mtaji wa kura ambazo zinatokana na yale ambayo ameyafanya kugusa mioyo ya Watanzania wengi.

Macho yangu yamekuwa shuhuda ya yale ambayo yamefanyika katika nchi yetu. 


Iko mahali ambako kila Mtanzania anajivunia, ndio kipindi ambacho sasa Tanzania imetoka kuwa nchi masikini, tuko uchumi wa kati chini ya utawala wa Dk.Magufuli. Kwa hilo tu anakosaje kuwa Rais wa Tanzania.


Wakati natafakari kazi kubwa na nzuri ambayo imefanywa na Rais Magufuli katika kipindi cha miaka mitano, kuna wakati natafakari tu, hivi huyu mzee wa watu anafanya kampeni za nini? 


Watanzania wameshamuelewa na wanachosubiri ni Oktoba 28 tu , wamchague aendelee na kazi.Lakini nakumbuka kumbe ni Katiba ndio inazungumzia masuala ya Uchaguzi Mkuu sambamba na kamepeni za kuomba kura.


Kote ambako Dk.Magufuli anakutana na maelfu ya Watanzania ambao wanafika kwenye mikutano yake kumsikiliza na sio kumsikiliza tu wanamuelewa. Wagombea wa upinzani kuna watu wanakwenda kwenye mikutano yao lakini mpaka mkutano unamalizika hawajui washike lipi , waache lipi.Kwa Dk.Magufuli anazungumza, anasikika na kisha Watanzania wanamuelewa.


Nikiri kwa kazi ambayo Dk.Magufuli ameifanya sina shaka na ushindi wake, sina shaka hata kidogo. Amefanya mengi sana , aliyoyafanya ndio yanayosababisha watu kufurika kwenye mikutano yake ya kampeni.


Yaliyofanywa na Dk.Magufuli yanazungumzwa na kila mtu.Yanazunguzwa na akina siye pangu pakavu tia mchuzi, yanazungumzwa na wasomi, yanazungumzwa na wakulima, yanazungumzwa na wafanyabiashara, yanazungumzwa na wafanyakazi, yanazungumzwa na wafugaji.


Yaliyofanywa na Dk.Magufuli yanazungumzwa na mataifa ya nchi, yanazungumzwa na wasiosoma kama mimi, yanazungumzwa na kila mtu.Hata waliokuwa wakihutubia madini yetu nao sasa wanazungumza yanayofanywa na dk.Magufuli.


Ndio yanazungumzwa na kila mtu.

Hata hivyo kati ya wote hao ambao tunazungumza kuhusu yale ambayo Dk.John Magufuli ameyafanya kuna Mtanzania mwenzetu mmoja amekuwa akiyafafanua vizuri sana.Kuna binti amezungumza vizuri, amezungumza kwa hatua.


Ametumia sanaa ya wimbo kuzungumza mambo yaliyofanywa na Rais Magufuli.Unajua anaitwa nani huyo? Ni Zuchu, mtoto wa Hadija Kopa, ameimba nyimbo ambayo naamini hata akina Tundu Lissu na Membe huku waliko nao uwa wanaisikiliza.Imesema kila kitu.

 

Zuchu kupitia nyimbo yake anaeleza hivi.Hebu fuatilia vizuri maisha ya wimbo wake unaoitwa Tanzania ya Sasa, Ujue anasemaje ? Anasema hivi fuatilia hatua kwa hatua...Anaanza hivi ;We mama njoo, Njoo uone nchi ilivyobadilika, Tanzania ya leo, Imejengwa imejengeka ...pta Ubungo Tazara Za juu barabara tayari zinatumika, Reli yenye viwango bora  Standard Gauge karibu inakamilika.


Tanzania ya sasa mama, hai mama...Ya Magufuli mama, hai mama, Inawaka waka mama, hai mama, Inapendeza sana, hai mama

Tanzania ya sasa mama, hai mama, Ya CCM mama, hai mama, Inawaka waka mama, hai mama, Inapendeza sana.


Nasema jua lile literemke mama, Jua lile literemke mama, Nasema wapinzani watetereke sana, Wapinzani watetereke sana

Jamani jua lile literemke mama, Jua lile literemke mama, Wabaki wapinzani watetereke sana, Wapinzani watetereke sana.


Wazee watoto, wanawake hospitali bure, Bure Magufuli huyoo, Elimu ya msingi pamoja na sekondari bure...

Bure Magufuli huyoo. CCM hai, hai, hai, hai, Magufuli hai, hai, hai, hai, Wapinzani wamekaa, kaa, kaa, kaa kaa

Wamekaa, kaa, kaa, kaa kaa

Doctor Sheni hai, hai, hai, Mama Samia hai, hai hai, hai


Wapinzani wamekaa, kaa, kaa, kaa kaa, Wamekaa, kaa, kaa, kaa kaa

Majaliwa hai, hai, hai hai, Nabashiru hai, hai, hai hai

Wapinzani wamekaa, kaa, kaa, kaa kaa, Wamekaa, kaa, kaa, kaa kaa

Tanzania ya sasa mama, hai mama, Ya Maghufuli mama, hai mama, Inawaka waka mama, hai mama, Inapendeza sana, hai mama, Tanzania ya sasa mama, hai mama


Ya CCM mama, hai mama, Inawaka waka mama, hai mama, Inapendeza sana

Nasema jua lile literemke mama, Jua lile literemke mama,

Nasema wapinzani watetereke sana, Wapinzani watetereke sana

Jamani jua lile literemke mama, Jua lile literemke mama


Wabaki wapinzani watetereke sana, Wapinzani watetereke sana

Mzee Mangula hai, hai, hai hai, Polepole hai, hai, hai hai

Wabunge wote hai, hai, hai hai, Kamati kuu hai, hai, hai hai

Wajumbe wa nurse hhai, hai, hai hai, Wenye viti wa mitaa hai, hai, hai hai, Wenye vituo vitongoji hai, hai, hai hai


Mabalozi hai, hai, hai hai

CCM hai, hai, hai, hai, Magufuli hai, hai, hai, hai

Wapinzani wamekaa, kaa, kaa, kaa kaa, Wamekaa, kaa, kaa, kaa kaa

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...