Na Karama Kenyunko Michuzi TV

WAFANYABIASHARA watatu wa Kariakoo, walinzi wa Suma JKT na wengine sita, wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na mashtaka matano likiwemo la kula njama na kuiba mali yenye thamani ya zaidi ya Sh. M.94

Katika hati ya mashtaka iliyosomwa mahakamani hapo na wakili wa serikali Mwandamizi Wankyo Simon akisaidiana na wakili wa serikali Mwandamizi Credo Rugaju  imewataja washtakiwa hao kuwa ni, Rashid Mwinyimkuu, Noela Msangi na Athumani Sadick wafanyabiashara Kariakoo.

Wengine ni Said Juma na Rajabu Mrisho walinzi wa Suma JKT,  Hamis Selemani, fundi bomba, Florian Kalibata, Mkulima, Godfrey Mambosho mfanyabiashara, Ernest Kongwa, dereva Jafari Makekela na Kimbali Ally.

Akisoma hati ya mashtaka, Credo amedai katika kosa la kwanza kuwa  siku na mahali pasipojulikana mwaka huu ndani ya jiji la Dar es Salaam,  washtakiwa Juma, Mrisho, Selemani,Kalibata, Mambosho, Kongwa Makekela na Ally  walikula njama ha kutenda kosa la kuvunja jengo na kutenda kosa kubwa.

Katika shtaka la pili imedaiwa Julia 26, 2020 huko Keko Magurumbasi Wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam  washtakiwa hao hao walivunja na kuingia kwenye ghala na kuiba vifaa mbali mbali vinavyotumika kwa ajili ya kuunganishia mabomba vyenye thamani ya Sh. 94,306,664.23 mali ya  kampuni ya Junako Tanzania Ltd.

Katika shtaka la tatu mshtakiwa Mwinyimkuu anadaiwa kukutwa akimiliki vipande 45 vya vifaa mbali mbali vya kuunganishia mabomba ya maji huku mshtakiwa Msangi akikutwa na vipande vinne na mshtakiwa Sadick alikutwa na vipande vitano vya mabomba hayo ua kuunganishia maji mali ambayo idhaniwayo kuwa ya wizi kutoka kampuni ya Junako Tanzania Ltd.

Hata hivyo washtakiwa wamekana kutenda makosa hayo na kesi hiyo imeahirishwa hadi Septemba 23, mwaka huu.

Kwa mujibu wa upande wa mashtaka upelelezi katika kesi hiyo bado haujakamilika.

 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...