Na Said Mwishehe, Michuzi TV-Geita
WAGOMBEA ubunge katika Mkoa wa Geita wamemhakikishia mgombea urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi(CCM) Dk.Jon Magufuli kwamba kazi kubwa na nzuri ambayo ameifanya ya kupeleka maendeleo katika mkoa huu, wananchi wote wameshaamua kuwa kura za zote za ndio katika uchaguzi mkuu mwaka huu zinakwenda kwa Dk.Magufuli.
Wamesisitiza kwamba katika kipindi cha miaka mitano ya Serikali ya Awamu ya Tano chini ya uongozi wa Rais Dk.Magufuli huduma muhimu za kijamii zimeimarika huku wakielezea jinsi ambavyo mabilioni ya fedha ya fedha yametolewa kwa ajili ya majimbo mbalimbali ya mkoa huo na katika majimbo yao.
Wakizungumza leo kwenye mkutano mkubwa wa kampeni za mgombea urais wa CCM Dk.Magufuli uliofanyika Uwanja wa Kalangalala uliopo Mjini Geita, wagombea hao wamesema wananchi wa majimbo yote yaliyopo mkoa huo wameshaaamua kwamba katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 28, 2020 wanakwenda kumchagua Dk.Magufuli kwani wameridhishwa na maendeleo ambayo wameyapata chini yake.
Mgombea Ubunge Jimbo la Geita Mjini Costanine Kanyasu amesema wakati Dk.Magufuli anainga madarakani mwaka 2015 , Geita walikuwa wanakabiliwa na changamoto za uhaba wa maji, uhaba wa madarasa, huduma duni za afya, miundombinu ya barabara lakini baada ya Dk.Magufuli kuingia madarakani maendeleo makubwa yamefanyika.
“Wote tunakumbuka changamoto ya maji iliyokuwepo lakini baada ya Dk.Magufuli kuingia madarakani , visima 60 vya maji vimechimwa na tumepata Sh.bilioni 100 kwa ajili ya miradi mingine ya maji na hivyo maji yatapatikana katika maji kata zote 13.
Akielezea maendeleo ambayo yamepatikana , Kanyasu amesema katika sekta ya afya kuna mambo makubwa yamefanyika, wamejengewa hospitali ya Wilaya, zahanati mpya 22, kituo ca afya pamoja na kuongezwa kwa bajti ya dawa.Katika barabara nako kuna mengi yamefanyika ambapo Geita Mjini wamepata kilometa 22 za lami na kilometa 200 za barabara za kiwango cha changarawe.
Wakati katika elimu, Serikali katika kipindi cha miaka mitano imeendelea kuboresha miundombinu ya elimu ikiwa pamoja na kujengwa kwa shule za msingi mpya 13 , zimejengwa shule za sekondari na hivyo kupunguza msongamano wa wanafunzi.
Kwa upande wake Mgombea ubunge wa Chato Dk.Mardard Kalemani amesema amesimama mbele ya wananchi wa Geita kwa ajili ya kumuombea kura Dk.Magufuli kwa ajili ya kuhakikisha anarudi tena ili kuendelea kuleta maendeleo.
”Nimekuwa katika sekta ya nishati kwa kipindi cha miaka mitano kuna mengi yamefanyika katika umeme, tunakumbuka umeme ilikuwa ni kero ya muda mrefu.Hivi sasa hakuna tena mgao na Rais ameanza kujenga mradi mkubwa wa umeme katika bwawa la Julius Nyerere ambao utazalisha megewati 2115 ambao utakuwa umeme mwingi sana,”amesema Dk.Kalemani.
Amesema chini ya Rais Magufuli umeme umekwenda maeneo mengi ya vijijini kwani wakati anaingia madarakani umeme ulikuwa katika vijiji 2018 lakini hivi sasa vijiji 9653 vina umeme umeme, na kwababu hiyo Tanzania imekuwa ya kwanza Afrika kupeleka umeme vijijini huku akieleza kuwa bei ya kuunganishwa imeshuka hadi kufikia Sh.27000.
Wakati huo huo Mgombea ubunge Jimbo la Nyang’wale Hussein Kasu amesema wananchi wa jimbo lake wameshaamua Rais Magufuli miaka mitano tena kwasababu maendeleo ambayo yamepatikana katika utawala wake yanaonekana."Licha ya wilaya yetu kuwa mpya tumepewa Sh.bilioni kwa ajili ya maendeleo.
”Tumepata maendeleo mengi sana Nyang’ale, kila sekta imeboreshwa , tulikuwa hatuna hospitali ya Wilaya sasa tunayo, umeme umeshakwenda katika vijiji 44 kati ya vijiji 62 tulivyonavyo na kazi ya kusambaza umeme inaendelea.Tumepewa Sh.bilioni 11 kwa ajili ya mradi mkubwa wa maji na umekamilika kwa asilimia 90.
Kwa upande wake Mgombea ubunge jimbo la Mbogwe Emmanuel Maganga amesema “Kwa maendeleo ambayo yamefanyika wananchi hatuna sababu ya kuchanganya pumba na mahindi.Vipo vyama vingi vina maneno mengi sana, msije kupoteza muelekeo, tumchague Rais Magufuli,”amesema.
Wakati huo huo mgombea ubunge jimbo la Bukombe Dotto Biteko amesema”Leo ni siku kubwa kwa watu wa Gita, ni siku kubwa kwa watu wa Bukombe. Tulivyokuwa kabla ya Dk.Magufuli kuingia madarakani na leo hii ni tofauti, tuna maendeleo makubwa katika sekta mbalimbali.Tunazo barabara ya lami, wananchi wana umeme, Sh.bilioni tano zimetolewa kwa ajili ya maji, watu wa Bukombe walikuwa wanasema kama kuna mtu anastahili kupitishwa bila kuhangaika basi ni Dk.Magufuli,”amesema.
Mgombea ubunge jimbo la Geita Vijijini Joseph Msukuma amesema “Wananchi wa Geita katika jimbo letu tunaona kama ndoto, tunayo hospitali ya wilaya nzuri, mabarabara nzuri, wamepata fedha nyingi kuboresha shule, leo hakuna shida ya kuchimba madini.Wana Geita Oktoba 28 mwaka huu wote kwa pamoja twendeni tukamchague Dk.Magufuli.”
Wakati huo huo Mgombea ubunge jimbo la Busanda Tumain Magesa amesema Serikali ya Awamu ya Tano imewajengea hospitali ya wilaya, ujenzi wa miundombinu ya barabara, wanazo kata 13 zinachimba madini na wanayo masoko matatu ya kuuza madini.Kuna mengi yamefanyika Busanda.

Waziri wa Madini Doto Biteko akiwa na pacha wake Kurwa Biteko pamoja na wagombea Ubunge wengine wa CCM mkoa Geita.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...