Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, imewahukumu mwanamama Masse Uledi (43) na Nkinda Shekalage (34), waliokuwa wakitumia jina la Janet Magufuli kutapeli kulipa fidia ya Sh. Milioni 16 baada ya kukiri kutenda kosa hilo.

Pia mahakama imewahukumu kutumikia kifungo cha nje cha miezi saba kwa masharti ya kutotenda kosa lolote la jinai kwa muda huo.
Aidha mahakama hiyo imeamuru vifaa walivyokuwa wakivitumia washtakiwa kufanyia utapeli huo, ambavyo ni simu 12, kompyuta mpakato mbili, flashsisk tatu, modern mbili vitaifishwe na kuwa mali ya Serikali.


washtakiwa hao walikuwa wakikabiliwa na makosa matatu ambayo ni kuchapisha taarifa za uongo kwenye mtandao, kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu na kutakatisha.

Hata hivyo, mashtaka mawili dhidi yao yamefutwa na leo wamesomewa shtaka moja la kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu.


Hukumu hiyo imesomwa na Hakimu Mkazi Mwandamizi Augustina Mmbando kufuatia washtakiwa hao kukiri makosa yao baadavya kuingia makubaliano na Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP)

Akisoma hukumu hiyo Hakimu Mmbadndo amesema, mahakama imewataja hatiani baada ya kukiri wenyewe makosa yao

Awali walidaiwa kati ya Januari 20 na Machi 31 2020 jijini Dar es Salaam na katika maeneo mengine ya ndani ya Tanzania washtakiwa hao kupitia mtandao wa Facebook walichapisha ujumbe unaosema JANET MAGUFULI SACCOS "mpya mpya isome tafadhali mkopo yote ni online tuu! 
 
Na utapata ndani ya dakika 45 tu. Mikopo huanzia kutolewa kuanzia laki tatu hadi milioni ishirini. Kufuata utaratibu huu ili kupata mkopo ..... tuma namba za kitambulisho cha mpiga kura au NIDA na majina yako matatu kupitia namba 0685012921 kisha Piga namba hiyo ili upatiwe namba ya mhasibu ili kuweka akiwa hatimae kupata mkopo...", ambapo walifanya hivyo huku wakijua kuwa si kweli na walikuwa na lengo la kuipotosha jamii.

Pia kwa njia ya udanganyifu walidaiwa kujipatia Sh. 15,068 650 kupitia muamala wa simu iliyosajiliwa kwa jina la Adam Mamba huku akijua kuwa si kweli.

washtakiwa hao walijipatia kiasi hicho cha fedha huku wakijua kuwa fedha hizo ni zao la kosa la kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu.

Hata hivyo, washtakiwa hao wamelipa fidia na wameachiwa huru.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...