WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais ,Mazingira na Muungano na Mbunge wa Jimbo la Ilala Mussa Azzan Zungu anatarajiwa kuwa Mgeni Rasmi katika Fainali ya Timu ya Combine FC dhidi Kilambasi FC.
Mechi ya Fainali itachezwa Septemba 13 mwaka huu katika Uwanja wa Mhimbili jijini Dar es Salaam.
Combine FC Iliibuka mshindi wa goli nne na kuingia katika fainali iliyokuwa na mzunguko wa kutoana kwa timu sita.
Kiongozi Mkuu wa Timu hiyo Yunus Msanguka amesema kuwa Wana uhakika wa kuchukua kombe hilo kutokana na walivyojipanga katika fainali hizo.
Msanguka amesema kuwa hadi kufika hapo kwa timu ya Combine wamepigana sana na moja ni uwezo binafsi wa wachezaji kujituma.
Aidha amesema kuwa Wana uhakika timu ya combine FC kufika mbali katika mashindano mbalimbali yatakayo andaliwa.
Tumedhamiria na timu hii kuhakikisha tunakuwa na vijana wenye vipaji ambavyo vitatumika kama fursa ya ajira kwao.



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...