Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na U talii  Dkt. Aloyce Nzuki akitangaza Mikoa  23 ya  Tanzania Bara ya kuanzisha Bucha za Wanyamapori, huku Mikoa ya Songwe, Mara na Rukwa ikikosekana katika orodha ya kwanza.

Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na  Utalii  Dkt. Aloyce Nzuki akisalimiana na watumishi wa  TAWA makao makuu baada ya kufika katika ofisi hizo leo 25.09.2020
Baadhi ya watumishi wa makao makuu TAWA wakimsikiliza Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii leo 25.09.2020.


Na Farida Saidy, Michuzi TV, Morogoro

BAADA ya watanzania kusubri kwa muda mrefu kufunguliwa kwa bucha za Wanyayapori hapa nchini hatimaye Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt.Aloyce K.Nzuki, ametangaza rasmi maeneo ya  kuanzisha bucha za Wanyamapori.

Akitoa taarifa hiyo mbele waandishi wa habari leo katika Ofisi za makao makuu ya Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania( TAWA) Mkoani Morogoro, Katibu Mkuu huyo ametangaza Mikoa 23 ya Tanzania Bara ambayo itaanza kufungua Bucha za wanayapori.

Amesema kuwa Mikoa iliyosalia ikiwemo Mikoa ya Songwe, Mara na Rukwa nayo itapewa fursa ya kuuza kitoweo hicho baada ya kukamilika kwa utaratibu wa kiutendaji ambao umewekwa na mamlaka hiyo.

 Sambamba na uanzishwaji wa majengo ya bucha za Wanyamapori,Wizara imeweka vigezo vya Magari maalum yatakayotumika kubeba na kuuza Nyamapori(mobile butcher) katika maeneo mbalimbali nchini.

Hata hivyo ameeleza kuwa mpaka sasa TAWA imepokea jumla ya maombi 25 ya watanzania wanaokusudia kuanzisha bucha za Wanyamapori, na  amewataka watu kujitokeza kwa wingi na kuchangamkia fursa ya kutuma maombi ndani ya siku 14 kuanzia tarehe 25.09.2020 ili kuwahi kalenda ya vikao vya kamati ya kupitisha maombi,ambayo inakutana mara nne kwa mwaka.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...