Mgombea Urais na Mwenyekiti wa CCM,Rais Dk.John Magufuli 



Na Said Mwishehe,Michuzi TV-Dodoma


CHAMA Cha Mapinduzi(CCM) kimesema kuwa Uchaguzi Mkuu ungekuwa umefayika Jumatano ya wiki hii, mgombea wake wa Urais Dk.John Magufuli angeshinda kwa asilimia 89.5.


Akizungumza leo Septemba 25 mwaka 2020, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama hicho Humphrey Polepole aliyekuwa akitoa tathimini ya kampeni za Chama hicho ambapo amesema kampeni zao zinakwenda vizuri na wameshambulika kila kona ya nchi yetu.

"Tumekuwa tukifanya tathimini na hali ya mwenendo wa kampeni, uchaguzi mkuu ungekuwa umefanyika Jumatano ya wiki ya Septemba 23, mgombea wetu utafiti wa kisayansi ambao tumeufanya angeshinda kwa asilimia 89.5,"amesema Polepole.


Amesisitiza matokeo ya asilimia hizo ni kwa mujibu wa uchambuzi wa kisayansi."Matokeo haya ni kwa mujibu wa uchambuzi wa kisanyansi kama mnakumbuka tulianza kwa barabara lakini kwa sasa kuna kelkopta ili tufike kila mahali na kufika kwa urahisi."


Ameongeza kuwa helkopta hiyo itatumika katika maeneo mengine lakini asilimia kubwa mgombea wao wa urais atatumia barabara kukutana na wananchi lakini huko mbele ya safari watakuwa na mbinu mpya ya kufanya kampeni zao.Aidha Polepole amesema Mgombea urais wa CCM katika Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Dkt. Hussein Mwinyi atashinda kwa kishindo kwani anaendelea na kampeni zake vizuri.


Amefafanua Dkt. Mwinyi ameshafanya mikutano katika Visiwa vya Unguja na Pemba na mwitikio wa wananchi ni mkubwa, hivyo amebaki na deni la kuhakikisha anawaletea maendeleo makubwa kwa kwenda na kasi ya Dkt.Magufuli baada ya kumalizika kwa Uchaguzi Mkuu.


"Dkt. Mwinyi atamshinda yule babu kulee(Maalim Seif)kwa kishindo maana anatafuta kushinda lakini hawezi bali alichonacho ni tamaa ya madaraka ndio inamfanya agombee, wakae tayari kumtia moyo maana ushindi unakwenda CCM tena tutashinda mapema kabisa na kwa kishindo.

"Na yule mzee namwambia asinijaribu mimi maana hana mbio za kukimbizana, hivyo hawezi kushinda na anachoonekana anapenda sana  king’oling’oli, aache kama hataki tutamfundisha adabu,"amesisitiza Polepole.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...