Na Bakari Madjeshi, Michuzi TV
Klabu
ya Soka ya Al Ahly ya nchini Misri imeanza kuonyesha nia ya kutwaa taji
la Tisa la Michuano ya Ligi ya Mabingwa ya Afrika baada ya kuitandika
Wydad Athletic Club ya Morocco bao 2-0 katika mchezo wa mkondo wa kwanza
wa Nusu Fainali ya Michuano hiyo uliopigwa kwenye dimba la Mohammed V
nchini Morocco.
Mchezo
huo uliokuwa wa kuvutia dakika zote 90, Al Ahly waliokuwa chini ya
Kocha wao mpya, Pitso Mosimane walionyesha matumaini ya kufika Fainali
ya Michuano ya CAF kwa ngazi ya vilabu kwa kutandaza kabumbu safi
ugenini nchini Morocco.
Dakaki
za mwanzo tu, Al Ahly walionyesha matumaini hayo baada ya kupata bao
safi dakika ya 4 ya mchezo kupitia kwa Kiungo wake, Mohammed Magdy
ambaye alitumia makosa ya mabeki wa Wydad Casablanca waliokuwa katika
harakati za kuondoa hatari langoni mwao.
Wydad
Casablanca wakiwa nyumbani walipata penati dakika ya 42 ya mchezo
ambayo ingeweza kusawazisha bao hilo lakini kwa bahati mbaya, Penalti
hiyo iliyopigwa na Mchezaji, Yahya Jabrane iliondolewa na Golikipa wa
Al Ahly, Mohammed El Shenawy.
Dakika
ya 62 ya mchezo, Al Ahly walipachika bao la pili kupitia kwa Ali
Maáloul kwa mkwaju wa Penalti baada ya Beki wa Wydad kushika mpira
uliopigwa na Nyota wa Al Ahly, Junior Ajayi katika eneo la hatari.
Matokeo
hayo yatasubiri mchezo wa marudiano utakaopigwa Oktoba 23, 2020 mjini
Cairo nchini Misri, mchezo ambao utaamua mshindi ambaye atacheza
Fainali ya Michuano hiyo kati ya Zamalek au Raja Casablanca.





Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...