Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. John Mongella (wa tatu kushoto) akionesha nembo ya Benki mpya ya NCBA Tanzania wakati wa hafla ya chakula cha usiku kwa wateja na wadau wa benki hiyo, iliyofanyika jijini Mwanza mwishoni mwa wiki. Wengine ni Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya NCBA Tanzania, Margaret Karume (wapili kulia), Mkurugenzi wa Biashara na Huduma za Kidigitali wa Benki hiyo, Gift Shoko ( wa pili kushoto) Katibu Tawala mkoa wa Mwanza, Mhe. Emmanuel Tutuba na Kamishina Msaidizi wa Polisi mkoa huo, Muliro Jumanne Muliro.
Mkurugenzi wa Biashara na Huduma za Kidigitali wa Benki ya NCBA Tanzania Ltd, Gift Shoko akizungumza na wageni waalikwa waliohudhuria kwenye hafla ya chakula cha usiku kwa wateja na wadau iliyoandaliwa na Benki ya NCBA kwa ajili ya uzinduzi wa matawi mawili ya Benki hiyo yaliopo mkoani Mwanza.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. John Mongella akizungumza na wageni waalikwa waliohudhuria kwenye hafla ya chakula cha usiku kwa wateja na wadau iliyoandaliwa na Benki ya NCBA kwa ajili ya uzinduzi wa matawi mawili ya Benki hiyo yaliopo mkoani Mwanza.


=====  ========  ========

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza aitaka Benki ya NCBA kusaidia kwenye pamba, uvuvi, madini, viwanda, nishati na ufugaji 

Mwanza. NCBA Bank Tanzania Limited (NCBA) ilisheherekea hatua nyingine ya kihistoria ya ujio wake nchini kwa kuzindua matawi mengine mawili mapya mkoani Mwanza mnamo tarehe 2 Oktoba. Matawi haya yanapatikana Plot No 5 – Barabara ya Nyerere Road na Jengo la Kauma – Barabara ya Kenyatta. 

Hafla hii ni kati ya sherehe zinazoendelea za ujio wa Benki ya NCBA ambayo ni muunganiko wa hiari kati ya NIC Bank (T) Limited na CBA Bank (T) Limited ambapo huduma rasmi za taasisi hii mpya zilianza tarehe 8 Julai 2020 baada ya idhini ya Benki Kuu ya Tanzania. 

Uzinduzi huo ulianza kwa matembezi yenye nderemo na shangwe wakitamka kauli yao mbiu iitwayo GOR FOR IT kutoka kwa wafanyakazi wa NCBA kwenye mitaa na barabara ya jiji la Mwanza kutoka tawi lao lililopo kitalu namba 5 – Barabara ya Nyerere Road hadi jengo la Kauma – Barabara ya Kenyatta na baadae kukafanyika hafla ya jioni kuhitimisha uzinduzi huo. 

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza aliekuwa Mgeni Rasmi katika matukio yote mawili alitoa wito wake kwa benki ya NCBA kwa kuelezea sekta muhimu za uchumi mkoani Mwanza wenye idadi ya watu takriban milioni moja. Alikaririwa akisema, ‘…pia tunajivunia rasilimali watu kwani Mwanza ni mji wa pili kwa ukubwa nchini Tanzania wenye takriban watu milioni 1. Ni moja wapo ya miji inayokuwa kwa kasi kubwa zaidi kutokana na fursa, rasilimali na shughuli za kiuchumi katika sekta zote nilizo-zitaja, iwe madini, kilimo, mifugo, uvuvi na viwanda’. 

‘Mwanza inategemea sana shughuli za uvuvi, ambayo inaongoza kwa mapato ya fedha ikiwemo zile za kigeni. Jiji hili ni makao ya viwanda 13 vya kusindika samaki zenye uwezo wa kusindika karibu tani 1,065 za samaki kwa siku, hivyo kutoa mchango mkubwa unaomarisha uchumi wa mkoa huu kwa kutoa ajira mbali mbali kwa wananchi’. 

Mkuu wa Mkoa aliendelea kusisitiza kuhusu umuhimu wa kusaidia maendeleo ya sekta ya biashara kwa viwanda vidogo, vya kati na vikubwa. Alisema, ‘Ni imani yetu kuwa Benki ya NCBA kama taasisi ya fedha itakuwa moja ya washirika bora, watakaowezesha wafanyabiashara wadogo, wa kati na wakubwa kusonga mbele katika hatua mpya ya maendeleo na kukuza pato la Taifa’. 

Halikadhalika, Mkuu wa Mkoa hakusita kuipongeza benki ya NCBA kwa ujio wao wa kihistoria kwenye Mkoa huo na Taifa kwa ujumla. Alisikika akisema, ‘Ujio wenu kama benki mpya utasaidia sana kuanzisha na kukuza miradi mipya pamoja na kutoa programu mpya za kifedha zitakazokuza uwezo wa kiuchumi wa watu wa Mwanza na kuleta thamani zaidi katika vipaumbele vya uchumi na shughuli za uzalishaji katika mkoa wa Mwanza’. 

Mkurugenzi Mkuu na Afisa Mkuu Mtendaji wa benki ya NCBA, Bi Margaret Karume aliwahakikishia wadau, wageni na wateja kuwa Benki inatoa huduma bora za kiwango cha kimataifa mahali popote walipo. Alisema, ‘Ninayofuraha ya kuwa-ha-ki-kishia wateja wetu wote kuwa wapo huru kutembelea tawi lolote lile la NCBA Bank ili kupata huduma zile zile bora kwa kiwango cha kimaitaifa, iwe hapa Mwanza ama katika miji mingine au visiwani Zanzibar. Pia, kufuatia muunganiko wetu, wateja wana uhuru na urahisi wa kutumia mashine yoyote ile ya ATM yenye nembo ya NCBA Bank ukiwa Mwanza, Arusha, Zanzibar, Dar es salaam ama katika nchi jirani za Kenya, Uganda, Rwanda, na Ivory Coast’. 

Bi. Margaret Karume, alimshukuru Mkuu wa Mkoa pamoja na waheshimiwa wageni waalikwa kwa utayari wao wa kuiunga mkono Benki ya NCBA. Margaret Karume alisisitiza umuhimu kwa Benki ya NCBA kuunga mkono mageuzi ya kiuchumi ya Mkoa wa Mwanza na Taifa kwa ujumla. Alisema, ‘Benki ya NCBA inaleta kwa pamoja ubora wa dunia mbili. Kuchanganya nguvu za taasisi mbili za awali zinaifanya benki ya NCBA kuwa benki kubwa na yenye nguvu kifedha, yenye utaalam na uwezo mkubwa unaowa-weka wateja wake mstari wa mbele katika safari yao ya mafanikio. 

‘Kama benki kubwa na imara, benki ya NCBA itahakikisha tunawashika mkono wateja wetu na kutoa huduma za kipekee za kifedha zitakazo-wawe-zesha katika safari yao ya mafanikio. NCBA ni benki inayokuhudumia vilivyo leo, kwa ajili ya mafanikio yako ya kesho’. 

Alimalizia kwa kusema, ‘Katika kuwahudumia wateja wetu na kufikia matarijio ya maendeleo ya kiuchumi hapa Mwanza, tunatarajia kuwa na mazungumzo ya kina na wateja wetu pamoja na wadau mbalimbali wa biashara na mandeleo ili kutengeneza mikakati imara itakayo-kidhi malengo yetu ya kuhamasisha kila mmoja kufikia malengo’. 

Uzinduzi wa matawi haya mawili mkoani Mwanza ni miongoni mwa matawi 12 mapya ya Benki ya NCBA kote nchini baada ya uzinduzi wa Makao Makuu na Tawi Kuu mkoani Dar es Salaam mnamo tarehe 19 Agosti 2020, iliyofuatiwa na uzinduzi wa matawi mawili jijini Arusha mnamo tarehe 19 Septemba na tawi moja visiwani Zanzibar tarehe 26 Septemba.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...