Ofisa Uhusiano wa Benki ya Biashara ya Taifa (NBC) tawi la Moshi, Neema Soka akipokea cheti kutoka kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Gerald Kusaya wakati wa maonesho ya Kawaha (Kahawa Festival) yaliyofanyika Moshi- Kilimanjaro.Kulia ni Katibu Tawala Mkoa wa Kagera, Profesa Faustine Kamuzola.Benki hiyo ni mmoja wa wadhamini wakuu wa maonesho hayo ambayo yalifanyika kwa siku tatu.
Ofisa Uhusiano wa Benki ya Biashara ya Taifa (NBC) tawi la Moshi, Neema Soka akimueleza jambo Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Gerald Kusaya alipotembelea banda la benki hiyo kufahamau namna ambavyo benki hiyo inasaidia sekta ya kilimo wakati wa maonesho ya Kahawa yaliyofanyika mjini Moshi. 
Ofisa Uhusiano wa Benki ya Biashara ya Taifa (NBC) tawi la Moshi, Neema Soka akitoa maelekezo kwa baadhi ya waliotembelea banda la NBC katika maonesho ya Kahawa (Kahawa festival) yaliyofanyika Moshi-Kilimanjaro.Benki hiyo ni mmoja wa wadhamini wakuu wa maonesho hayo ambayo yamefanyika kwa siku tatu mfululizo. 

……………………………………………… 

Moshi.Wizara ya Kilimo imepongeza juhudi mbalimbali zinazofanywa na benki ya Biashara ya Taifa (NBC) katika uwezeshaji wa wakulima kupitia mikopo na bidhaa mbalimbali ikieleza kuwa hatua hizo zitawakomboa wakulima wengi dhidi ya umasikini hapa nchini. 

Hayo yalisemwa wakati wa uhitimishaji wa maonesho ya kwanza ya Kahawa yaliyofanyika Mjini Moshi na kuhusisha wadau mbalimbali wa sekta ya kilimo na fedha ili kusherekea siku ya kahawa Duniani (International Coffee Day). 

Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Gelard Kusaya alisema taasisi za fedha zina mchango mkubwa katika kuendeleza sekta ya kilimo kupitia uwezeshaji kwa wakulima na wafanyabiashara kwa njia ya mikopo yenye riba nafuu. 

Kusaya alisema Wizara imefurahishwa sana na huduma ya ‘NBC Shambani’ na kwamba itakuwa na msaada mkubwa kwa wakulima kufanya kilimo-biashara ili waweze kuona tija zaidi. 

NBC Shambani ni huduma maalumu kwa wakulima inayowawezesha kufungua akaunti za vikundi (Amcos) au akaunti ya mkulima mmoja mmoja bila gharama za uendeshaji. 

“Mkulima anayetaka kujikita katika kilimo biashara ni lazima awezeshwe katika suala la fedha, mikopo mnayoitoa tunaamini inakuwa na faida kubwa kwa mkulima na mkulima ataweza kuzalisha zaidi,” alisema Kusaya. 

Meneja wa NBC Tawi la Moshi, Lazaro Mollel alisema maonesho hayo yamekuwa na faida kubwa katika kufahamu mahitaji ya wakulima hasa wakulima wa zao la kahawai li kuongeza ubunifu wa bidhaa. 

Amesema benki hiyo imeleta huduma maalumu kwaajili ya wakulima iitwayo NBC Shambani ambayo inawawezesha wakulima kufungua akaunti za vikundi (Amcos) pamoja na akaunti ya mkulima mmoja mmoja bila gharama za uendeshaji. 

“Huduma ya NBC Shambani inawalenga wadau wote wa kilimo wakiwamo wasambazaji, wakulima, wauzaji wa pembejeo na pia inatoa fursa kwa wakulima wanaofanya kazi kwenye vikundi vya ushirika (Amcos) kufungua akaunti ya kikundi kufungua akaunti ya pamoja na ya mtu mmoja mmoja ambazo uendeshaji wake ni bure,” amesema. 

Katika maonesho hayo, NBC imeweza kukabidhiwa tuzo ya mdhamini mkuu wa maonesho hayo ambayo ni ya kwanza kufanyika nchini Tanzania.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...