Na Lusajo Frank, DSJ 
BWENI la shule ya sekondari inayomilikiwa na taasisi ya dini ya Kiislamu ya African ilitoko kiloleni mkoani Kilimanjaro limeteketea moto usiku wa kuamkia leo Octoba 9.

Kikosi cha zimamoto kanda ya Kilimanjaro kilifanikiwa kudhibiti moto huo, huku jeshi la polisi mkoani hapo linaendelea na uchunguzi kubaini chanzo cha moto huo.
 
"Tulipata wito kwamba kuna moto katika shule ya sekondari ya African Muslim na tulipofika tukakuta moto ni mkubwa sana ni jengo la bweni la ghorofa moja na moto ulikuwa umeanzia kwenye moja ya chumba ambacho kinatumika kama stoo." Amesema Inspekta Jeremiah.

Inspekta Jeremiah ameongeza kuwa "Kwenye tukio hilo hakuna majeruhi wala kifo kwa sababu wanafunzi waliondolewa mapema na kupelekwa sehemu salama, vitu vilivyoungua ni nguo zao, vitanda na madaftari, chanzo hakijabainika kwa sababu kumekuwa na mlolongo wa shule kuungua na hii ni mara ya tatu".

Aidha, matukio ya kuteketea moto shule za kiislam yamezidi kushika kasi katika mikoa mbalimbali hapa nchini.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...