Na Jeshi la Polisi nchini

MKUU wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro ameelezea hali ya kisiasa nchini imeendelea kuimarika hasa wakati huu wa kampeni za uchaguzi mkuu na wananchi wengi wamekuwa watulivu licha ya kuwepo kwa baadhi ya watu wachache walioandaliwa na baadhi ya viongozi wa vyama vya kisiasa kwa ajili ya kufanya vurugu na kujiingiza kwenye uhalifu.

IGP Sirro aliyasema hayo jana jijini Dar es salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari na kuwataka baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa kufanya masuala ya siasa na kuacha kuwatumia vijana na kuwaingiza kwenye uhalifu.

Hata hivyo, IGP Sirro alisema kuwa, yeyote atakayebainika atachukuliwa hatua za kisheria huku akiwataka wananchi kuepuka vishawishi vya kujiingiza kwenye uhalifu na kubeba matatizo ya wengine kwa kupata shida kutoka kwa baadhi ya wanasiasa wasiowatakia mema na kushindwa kutimiza ndoto zao, alisema.

Aidha, Kuhusu upigaji wa kura Zanzibar, IGP Sirro alisema, wapo baadhi ya watu wanaohamasisha baadhi ya watu au kikundi cha watu kuvunja sheria wakati wa zoezi la upigaji kura kinyume cha sheria, kanuni na taratibu zilizopo na kwamba zoezi la upigaji kura litafanyika kwa mujibu wa tarehe iliyopangwa na litafanyika kwa amani na utulivu na kuwapata viongozi watakaowataka.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...