Na Said Mwishehe,Michuzi TV

CHAMA Cha Mapinduzi( CCM) kimesema kwamba leo Oktoba 14 mwaka huu wanamliza awamu ya tano ya kampeni zao na kuzindua rasmi awamu ya sita ya kampeni zao ambazo ndio za salama huku kikitumia nafasi hiyo kuwaomba wakazi wa Dar es Salaam kuhakikisha Oktoba 28 mwaka huu wanamchagua mgombea urais wa Chama hicho Dk.John Magufuli.

Akizungumza leo Oktoba 28,2020 mbele ya maelfu ya wananchi wa Majimbo ya Kawe na Kinondoni jijini Dar es Salaam, Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Dk.Bashiru Ally amesema ratiba yao imepangwa kimkakati.

Dk.Bashiru amesema awamu ya sita ambayo wanaizundua leo kwa Mgombea wao kufunga kampeni zake jijini Dar es Salaam na kuelekea mikoa mingine ,ndio awamu ya lala salama ambayo wana CCM wanajipanga zaidi kuelekea Oktoba 28 ambayo ni siku ya uchaguzi mkuu.

"Leo tunamaliza awamu ya tano na kungia awamu ya sita ya kampeni zetu, bdii awamu ya kupanga mawakala katika vituo vya uchaguzi, ndio awamu ya kutafuta wapiga kura, ndio awamu kuelekeza wapiga kura jinsi ya kupiga kura, awamu ya mabalozi wetu kutafuta kura na ndio wakati wa kuchukua  silaha zetu zote. Ndio awamu ya lala salama,"amesema Dk.Bashiru.

Hata hivyo amesema wakati wakiendelea na kampeni zao,kuna mgombea urais wa upinzani amekuwa akijifanya anaijua vizuri ratiba ya mgombea urais wa CCM, hivyo wamemtaka mgombea huyo aache kugusa mitambo ya ushindi wa Chama hicho

"Mgombea hu yo  anajifanya anapanga ratiba ya mikutabo ya mgombea urais wa CCM,n kwa jinsi anavyoijua ratiba yetu tunadhani anakaibia kuja CCM, tunamkaribisha.Tunachotaka kusema mwaka huu wapinzani watachapwa sana, CCM  na mgombea wetu wa urais tunakwenda kushinda kwa kura nyinyi Oktoba 28 mwaka huu,"amesema Dk.Magufuli.

Ametumia nafasi hiyo kufafanua Dk.Magufuli katika uchaguzi mkuu mwaka huu ndio mgombea mwenye kazi ngumu kwani anafanya kazi zaidi ya moja ba zote amezifanya vizuri.

Pamoja na hayo amesema kuwa Jiji la Dar es Salaam ndilo kitovu cha ukombozi kwa nchi za barani Afrika, Dar es Salaam ndio wakombozi wa Taifa la Tanzania kiuchumi kwani hata mapato mengi yatokanayo na kodi jiji hilo linaongoza.Pia hata katika idadi ya wapiga kura Dar es Salaam ndio inaongoza kuwa na wapiga kur wengi kulko sehemu nyingine yoyote nchini.

"Tuhakikishe katika Oktoba 28 mwaka huu thugs Dk.Magufuli ashinde kwa kishindo, Tuchague wagombea ubunge na madiwani wa CCM,"amesema Dk.Bashiru na kuongeza Dk.Magufuli amesimama imara kuleta maendeleo ya nchi yetu hana wa kushindana naye na wala hakuna anayemfikia kwa sifa alizonazo kwa nafasi ya urais.

Kuhusu kumbukizi ya Hayati baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere ambaye aliyefariki dunia Oktoba 14,mwaka 1999 na kwamba ikifika mwaka 2022 Mwalimu Nyerere atakuwa anafikisha miaka 100 tangu atoke kwenye tumbo la mama yake.

"Mwalimu Nyerere anatimiza miaka 21 ya kifo chake, na itakapofika mwaka 2022 atakuwa anafikisha miaka 100 tangu azaliwe.Mwalimu Nyerere alisema bila CCM imara nchi itayumba na chini ya Dk.Magufuli CCM iko imara sana na anaishi katika maono ya Mwalimu Nyerere,"amesema Dk.Bashiru.

Amesema kwa Dk.Magufuli amekuwa akiishi katika maono ya Mwalimu Nyerere na amekuwa na sifa lukuki na miongoni kwa sifa hizo ni namna ambavyo amekuwa akisimamia rasilimali za nchi na tukio la jana la kupokea gawio la Sh.bilioni 100 kutoka sekta ya madini imethibitisha kwa vitendo Rais Magufuli anavyosimamia vema rasilimali zq nchi.

" Dk.Magufuli ana sifa ya kufanya kazi na maendeleo na hata katika mahusiano ya watu ni.makubwa chini ya uongozi wako, umekuwa ukisema maendeleo hayana Chama bali ni ya watu,"amesema.

 

 Mgombea Urais kupitia Chama cha Mapinduzi CCM Rais Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Wananchi wa Jimbo la Kawe katika mkutano wa Kampeni za CCM zilizofanyika katika uwanja wa Tanganyika Packers uliopo Kawe, Kinondoni mkoani Dar es Salaam leo tarehe 14 Oktoba 2020.

Wananchi wa Jimbo la Kawe wakiwa wamefurika katika Uwanja wa mkutano wa Tanganyika Packers kumsikiliza Mgombea Urais kupitia Chama cha Mapinduzi CCM Rais Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 14 Oktoba 2020.

Mgombea Urais kupitia Chama cha Mapinduzi CCM Rais Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwasili katika uwanja wa Tanganyika Packers kwa ajili ya kuwahutubia wananchi wa Jimbo la Kawe leo tarehe 14 Oktoba 2020.

 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...