*Aweka wazi jinsi atakavyoshughulikia changamoto ya ajira kwa vijana
Na Said Mwishehe,Michuzi TV
RAIS Dk.John Magufuli ametoa maagizo kwa Waziri pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji kuhakikisha inapofika Desemba mwaka huu maji yawe yanatoka katika maeneo ya Kinyerezi, Bonyokwa na Kifuru bikini Dar es Salaam huku akisisitiza hiyo ndio amri kwao na atafuatilia.
Akihutubia maelfu ya wananchi wa Wilaya ya Ilala kutoka majimbo ya Segerea,Ilala na Ukonga jijini Dar es Salaama wakati wa mkutano wake wa kampeni uliohudhuriwa na maelfu ya wananchi, Dk.Magufuli mbali ya kuzungumzia mafanikio ambayo yamepatikana katika kipindi cha miaka mitano iliyopita tangu aingie madarakani,amesema anafahamu na changamoto zilizopo katika majimbo hayo.
Amesema changamoto mojawapo ni uhaba waa maji safi na salama katika maeneo ya Kinyerezi,Bonyokwa na Kifuru ambapo amefafanua kuwa kwamba yote anayozungumza yapo kwenye Ilani ya uchaguzi."Nafahamu kuna kero ya maji Kinyerezi, Bonyokwa na Kifuru, tumeshatenga Sh. bilioni 7.3.Pia tutajenga tanki kubwa Pugu.Wakuu wa wilaya na mikoa, ma-das nataka Desemba wakati wananchi wanasherehea sikuu ya Krisimas wawe wanakunywa na maji ambayo yatakuwa yamefika hapa.
"Na kama kuna Waziri wa Maji na Katibu Mkuu wanisikilize mimi , ndio amri yangu, ndio maana nataka mniletee wabunge hawa ili wawe wananiambia kama maji yamefika au bado. Nataka hii changamoto kukosekana kwa maji ifike mwisho, nafahamu maeneo mengi maji yanapatikana na miradi inaendelea kutekelezwa,"amesema Dk.Magufuli.
Wakati huo huo amesema anafahamu bado kuna changamoto ya ya ubuvu wa miundombinu ya barabara katika maeneo mbalimbali ya Ilala,Segerea na Ukonga."Nafahamu hata hapa Kinyerezi bado kuna chagamoto ya umeme, siwezi kushindwa kuleta umeme.Nafahamu kuna mgogoro wa kati ya hifadhi na wananchi wa kazi Mzumbw na Zingiziwa, najaribu tu kuelezea kwamba Serikali ya Chama Cha Mapinduzi imejipanga kuwatumikia watu wote bila kujali vyama , dini wala kabila zoa na hiyo ndio maana ya hapa kazi tu.
"Ninachotaka kuwambia ndugu zangu mradi wa umeme wa Kinyerezi I na Kinyerezi II tumetengeneza umeme zaidi ya ule uliokuwepo zamani, hivyo haiwezekani umeme unatoka hapa halafu watu wake hawana umeme.Tumepanga pia kuboresha mazingira ya biashara ya wakubwa na wadogo, na Tanzania ni ya wote ,wafanyabiashara wadogo na wakubwa, nataka kuwambia nitawabeba kweli kweli,"amesema Dk.Magufuli.
Ametumia nafasi hiyo kuelezea mipango aliyonayo katika kuwasaidia wanawake,vijana na walemavu na kufafanua katika eneo la kusaidia wanawake kila mara anamfikiria mama yake ambaye sasa yuko kitandani kwa zaidi ya miaka miwili, hanyanyuki, na chakula analishwa kwa mpira kutokana na maradhi ya kupooza mwili.
"Wanawake wanateseka sana kwenye urithi, nitatembea na akina mama na ndio maana nimeamua kuwa na Mama Samia Suluhu ili aweze kunisaidia kunikumbusha katika kuwatetea akinana
Wakati huo huo ,Dk.Magufuli amezungumzia suala la ajira kwa vijana ambapo ameahidi kulitafutia ufumbuzi katika kipindi cha miaka mitano inayokuja huku akifafanua kama wameweza kujenga fly over,kununua ndege na meli basi hawezi kushindwa katika ajira za vijana ambao ndio taifa la kesho."Haya ninayozungumza sizungumzi kwa kufurahisha bali nasema ukweli, nataka Taifa hili lizungumzwe kama mataifa mengine ya Ulaya.
"Tuna gesi mpaka inamwagika, tuna aina nyingine ya gesi inapatikana Rukwa, tuna copa, tuna madini ya chumvi, maziwa tunayo, bahari tunayo, mlima mrefu tunao, hata mti mrefu kuliko yote duniani uko Tanzania.Nataka tuelewe tunakotoka, tuliko na tunakokwenda, tusije kupoteza muelekeo, Taifa ni tajiri hivyo maadui zetu watatumia mbinu za kila aina. Ninachowaambia tuendelee kuungana, Oktoba 28 msiseme Magufuli ameshinda, kushinda kwa Magufuli, kushinda kwa wabunge na madiwani kutokana na kwenda kupiga kura.
"Amkeni mapema siku hiyo mkapige kura kura , itakuwa Jumatano, sio Ijumaa , sio Jumamosi, wala sio Jumalipili ambazo ni siku takatifu za kumuomba Mungu, itakuwa Jumatano ambayo sio siku ya kufanya ibada. Nendeni mkatuchague wagombea wa CCM,"amesema Dk.Magufuli.
Home
SIASA
CHANGAMOTO UHABA WA MAJI KINYEREZI,BONYOKWA NA KIFURU DK.MAGUFULI ATOA MAAGIZO KWA WAZIRI, KATIBU MKUU WIZARA YA MAJI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...