* Mwalimu Nyerere alizingatia Utawala Bora na kuichukia rushwa
Na Jovina Bujulu-MAELEZO
KILA ifikapo tarehe 14, mwezi Oktoba, Watanzania wanakumbuka kifo cha
muasisi wa Taifa la Tanzania, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ambapo
mwaka huu atatimiza miaka 21 tangu afariki dunia.
Katika kipindi cha uongozi wake wa miaka 24, Taifa la Tanzania
limeshuhudia mafanikio lukuki katika nyanja za kilimo, viwanda, madini,
afya, elimu, maji na miundombinu. Mafanikio hayo bado tunayaona
yakiendelezwa na Rais wa Awamu ya Tano, Dkt. John Pombe Magufuli.
Mwalimu Nyerere ni miongoni mwa viongozi ambao waliweza kukidhi
matarajio ya Watanzania kwa kuzingatia maadili ya uongozi na kujenga
umoja wa kitaifa katika watu wa makabila zaidi ya 120 wenye dini
tofauti,hivyo kudumisha amani ya katika Taifa la Tanzania kumepelekea Tanzania kuitwa “ Kisiwa cha Amani”.
Ni kiongozi aliyebeba historia ya Taifa la Tanzania kwa mawanda mapana
kwa sababu huwezi kuitaja Tanzania bila kumtaja Mwalimu Nyerere.
Wakati wa utawala wake alichukia rushwa na akapitisha sheria kwamba
mtu akila rushwa, aliyetoa na aliyepokea wote watapata msukosuko.
Katika kuzingatia maadili ya uongozi, Mwalimu Nyerere alichukia sana
rushwa na aliipiga vita kwa nguvu zake zote. Hali hii ilijionesha awali
wakati wa chama kilicholeta uhuru Tanganyika mwaka 1961 wakati huo
kikiitwa Chama cha TANU na baadaye Chama Cha Mapinduzi (CCM,)
ambapo katika mojawapo ya ahadi za chama cha TANU ilikuwa inasema,
‘Rushwa ni adui wa Haki, Sitatoa wala Sitapokea rushwa.’
Rushwa ni adui wa haki, na ni kitendo kibaya kwa hiyo watu wanaofanya
kitendo hicho ni wabaya sana na kitendo hicho hakifungamani na adili za
jamii ya Watanzania kwani kinamfanya mwenye haki kunyang’anywa haki
yake.
Kwa kuweka ahadi hii kuwa mojawapo ya ahadi za TANU inaonesha jinsi
Mwalimu Nyerere alivyokuwa amedhamiria kuondoa suala la rushwa.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...