Jumuiya ya Afrika Mashariki na Serikali ya Ufaransa wamesaini makubaliano (MoU) kwa madhumuni ya kuendeleza ushirikiano wa kimkakati pamoja kudumisha ajenda za ushirikiano wa Jumuiya ya EAC.

Makubaliano hayo yamesainiwa makao makuu ya EAC jijini Arusha baina ya balozi wa Ufaransa nchini, Frederic Clavier na katibu Mkuu wa EAC Liberat Mfumukeko ambapo wameiangazia MoU kwa miaka 5  kushughulikia masuala mbalimbali ikiwemo nishati, mabadiliko ya tabia nchi, viwanda, maendeleo ya sekta binafsi katika Ukuzaji na uwekezaji, sekta ya fedha, ujenzi na ukuzaji miradi.

Awali balozi wa Ufaransa nchini akiwa ameambatana na Mkurugenzi AFD, Afrika Mashariki Christian Yoka walizungumza na katibu Mkuu EAC na kuziagiza pande mbili kushirikiana na kuendeleza sekta muhimu na uboreshaji wa maisha ya waafrika Mashariki.

Katibu Mkuu wa EAC, ameishukuru Serikali ya Ufaransa kwa kusaidia mipango inayoendelea ndani ya Jumuiya na kueleza kuwa EAC imepiga hatua kubwa na kueleza kuwa kabla ya Covid-19 biashara ndani ya Jumuiya ilikua na kuongezeka kwa kiasi kikubwa na hiyo ni pamoja na kupunguzwa kwa ada na vibali vya kuvuka mipaka pamoja na kutolewa kwa pasipoti mpya ya Afrika Mashariki inayotambulika kimataifa.

Imeelezwa kuwa fedha za AFD kwa Tanzania na ulimwengu mzima zinasaidia kuharakisha mabadiliko na maendeleo katika miradi mbalimbali ikiwemo Maji, elimu, afya, kilimo na maendeleo ya miji katika nchi 115.

Miaka ya AFD Tanzania imeimarisha miradi mbalimbali ya kimaendeleo ikiwemo afya, nishati pamoja na Maji na usafi wa mazingira na bado inaendelea kushirikiana na Serikali katika kuhakikisha maendeleo yanawafikia wananchi zaidi.

Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania,  Frederic Clavier (wa pili kushoto) na Katibu Mkuu wa jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), Liberat Mfumukeko (wa pili kulia) wakisaini Mkataba wa Makubaliano wa kuanzisha mfumo wa Ushirikiano ilikuwezesha ushirikiano wa kimkakati wa Chama. Mkataba huo umesainiwa mbele ya Mkurugenzi wa Kikanda wa Maendeleo ya Ufaransa, Christian Yoka (wa kwanza kushoto) na Afisa Mwandamizi wa EAC (wa kwanza kulia) mwishoni mwa wiki jijini Arusha.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...