Muonekano wa bodi la meli ya MV Mwanza inayojengwa jijini Mwanza na Mkandarasi GAS Entec kutoka Korea ya Kusini meli hiyo inayotarajiwa kukamilika mwakani itakuwa na uwezo wa kubeba abiria 1200, tani 400 za mizigo na magari zaidi ya 20 itakapokamilika.
Mtaalam wa masuala ya ujenzi wa meli Mhandisi. Beda Patrick akifafanua jambo kwa timu ya wahandisi toka Bodi ya usajili wa wahandisi nchini (ERB), walipokagua ujenzi wa meli hiyo jijini Mwanza.
Msajili wa wahandisi nchini Mhandisi. Patrick Barozi (mwenye
fulana nyekundu), akisisitiza jambo kwa wahandisi waliopata fursa katika mradi
wa ujenzi wa meli ya MV Mwanza kujifunza kikamilifu ili kupata ujuzi wa kutosha
katika ujenzi huo (wa kwanza kushoto kwake), ni Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana
Dkt. Phillis Nyimbi akifuatilia kwa
makini.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Meli nchini (MSL,) Bw. Erick
Hamis akifafanua jambo kwa timu ya wahandisi toka Bodi ya usajili wa wahandisi
nchini (ERB,) walipokagua maendeleo ya ujenzi wa meli ya MV Mwanza
inayotarajiwa kukamilika mwakani na kutoa huduma katika ziwa Victoria.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...