PROGRAMU ya 'Emirates Skywards' ya shirika la ndege la kimataifa la Emirates limefikisha miaka 20 katika utendaji kazi na ugunduzi kwa miongo miwili sasa na kuwanufaisha wateja kupitia safari na hiyo ni pamoja kutoa uzoefu kwa maelfu ya washiriki duniani kote.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na shirika hilo imeelezwa kuwa "Emirates Skywards" inawashiriki kutoka nchi ya zaidi 180 duniani huku "programu ya loyalty" ikiwa na wadau 200 yakiwemo mashirika 16 ya ndege, zaidi ya  hoteli 100, wadau wa fedha 33 na washirika saba wa kukodisha magari.

Wakiwa wameshikilia usukukani wa huduma za anga Emirates Skywards imeshinda tuzo zaidi ya 50 kwa miaka 20 iliyopita na tuzo hizo ni pamoja na Shirika linaoongoza kwa ubora wa usafiri wa anga ukanda kwa Mashariki ya Kati pamoja na Shirika linaoongoza kwa kurudisha fadhila kwa jamii.

Kupitia mafanikio hayo Emirates imetoa zawadi zaidi kwa wateja kupitia safari zao ambapo wateja wanaweza kununua zawadi na bidhaa mbalimbali kupitia safari zao.

Imeelezwa kuwa mwaka huu Emirates imeorodheshwa katika nafasi 10 likiwa shirika linaloongoza katika utoaji wa huduma bora za anga. 

Pia i meelezwa kuwa mwanzoni mwa mwaka huu Emirates kupitia programu ya'Loyalty'   walianzisha maelfu ya mbinu mpya za kununua bidhaa kwa njia ya mtandao katika maeneo pendwa ulimwenguni ikiwemo Dubai.

Wakiwa na wanachama wapatao milioni 27 duniani, wanachama 32,000 ambao walijiunga na programu hiyo katika miaka ya 2000 bado ni washiriki hai na katika maadhimisho ya miaka 20 Emirates Skywards itawazawadia wateja wenye tiketi za safari kuanzia Desemba 10 hadi Machi 31, 2021.

Emirates Skywards pia ina ubia na Dubai Mall ambapo washiriki kupitia Skywards hupata fursa ya kununua bidhaa kutoka kampuni zaidi ya 1300,  pamoja na kutembelea vivutio vikubwa na vingi zaidi ulimwenguni.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...