Mbunge Mteule wa Jimbo la Bumbuli Mkoani Tanga January Makamba amesema kuwa tunapokwenda kwenye uchaguzi wa kuamua hatima ya nchi ni lazima kuangalia mambo manne ikiwemo ubora wa sera na Ilani ,ubora wa Chama pamoja na ubora wa wagombea

Hayo aliyasema wakati wa Mkutano wa Kampeni  wa Mgombea Urais wa Chama Cha Mapinduzi CCM DK John Pombe Magufuli uliofanyika mjini Korogwe Mkoani Tanga, ambapo alisema jambo lingine la kuangalia ni rekodi na historia ya vyama katika kutekeleza ahadi zake nakuongeza kuwa historia ya CCM  ni kuaminiwa katika uongozi wa nchi na  kuongoza  nchi hii kwa  utulivu na usalama pamoja na ustawi kwa miaka yote.

Makamba  ambaye ni Katibu  Mstaafu  wa SUKI alisema kuwa katika vyama vyote vilivyosajiliwa  hakuna hata   Chama kimoja chenye sifa na sura  ya Kitaifa  kama Chama Cha Mapinduzi hivyo kwenye uchaguzi huu amewataka wananchi  waangalie ubora wa vyama na ubora wa wagombea.

Makamba ambaye anasubiri kuapishwa baada ya kupita bila kupingwa  alisema kuwa ubora wa sera na ilani ya CCM ukiilinganisha  na ilani ya vyama vyote,  ilani ya Chama cha Mapinduzi  imebeba mahitaji ,matamanio na matumaini ya watanzania  nakwamba  hata viongozi wao wanapoinadi  wanagusa mambo yote yanayowagusa moja kwa moja  wananchi.

" Hata  ukimsikia Rais wetu   John Magufuli anavyohutubia kwenye mikutano yake ya kampeni wala hatukani mtu, hamsemi mtu  wala hamlalamikii mtu bali anazungumza  mambo yanayogusa mahitaji  ya wananchi  na hiyo ni sifa nyingine aliyonayo Mgombea wetu wa Chama chetu "Alisema Makamba

Alisisistiza  kwamba  hakuna Chama kingine  katika uchaguzi  huu ambacho  kinarekodi  ya uongozi  wa nchi  au rekodi  ya  kutekeleza  mambo  yaliyoleta ustawi  kwa  watanzania hivyo wananchi wametakiwa katika uchaguzi huu wasiwe na mjadala  wa ubora  na historia  ya Chama kwani CCM ipo mbali  zaidi ukiilinganisha  na vyama vingine.

" Ndugu zangu  wagombea wetu waliochaguliwa na CCM kupeperusha bendera  ya chama  ngazi zote  wamechujwa  haswa  na hata Dk Magufuli  amepimwa ,kachujwa na ameonekana anastahili kupewa dhamana ya kuongoza  nchi yetu hivyo ifikapo October 28 twendeni tukamchague kwa kura nyingi "Alieleza Makamba ambaye kwasasa anasubiri kuapishwa baada ya kupita bila kupingwa.

Alisisistiza kuwa wakimchagua Rais Magufuli tena ili aongoze miaka mitano ijayo  anaimani yale mambo ambayo hayajakamilika  yatakamilika na yale ambayo wanayahitaji  na hayajaanza yataanza.

Hata hivyo alisema kuna mambo makubwa yamefanyika chini ya uongozi wa  Magufuli  nakwamba chama Cha Mapinduzi  kimesimamia Serikali na Sasa zaidi ya zahanati 20 zinajengwa  kwa mpigo katika Jimbo la Bumbuli .

Aliongeza kwa kusema kuwa hata barabara ya kutoka Soni hadi Bumbuli itajengwa kwa kiwango Cha lami kwani tayari imeshaingizwa kwenye ilani na ipo ukurasa wa 74 hivyo wanabumbuli wasifanye makosa bali siku ya uchaguzi wajitokeze kwa wingi kuichagua CCM  ili imalize ahadi zake.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...