Mwenyekiti wa UVCCM Taifa na
mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Kheri James akibadilishana mawazo na
Mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Arusha Omary Lumato walipokuwa Jana katika
mkutano wa hadhara uliofanyika kata ya Kiranyi iliopo ndani ya
halmashauri ya Arusha DC mkoani Arusha (picha na Woinde Shizza ,ARUSHA)
Mwenyekiti wa UVCCM Taifa na
mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Kheri James(MCC)akihutubia mkutano wa
hadhara wa kampeni za kumnadi Mgombea ubunge wa jimbo la Arumeru
Magharibi Noah Saputu katika mkutano wa hadhara uliofanyika kata
ya Kiranyi iliopo ndani ya halmashauri ya Arusha DC mkoani Arusha
Mwenyewe wa UVCCM mkoa Arusha
Omary Lumato Akiongea akimuombea kura Rais Magufuli katika mkutano wa
adhara uliofanyika katika kata ya Kiranyi

wananchi wa Kijiji Cha Kiranyi wakiwa wamenyoosha mikono juu ishara ya kumpigia Kura Rais Magufuli
…………………………………………………………………………………………………
Na Woinde Shizza , Arusha
Mwenyekiti wa UVCCM taifa Kheri James amewasii
wananchi wa Jimbo la Arumeru magharibi kuichagua CCM kwasababu ndio
Chama pekee kilichoahidi katika Ilani yake ita hakikisha inawezesha
miradi mikubwa ya kimkakati itakayo zalisha Ajira kwa vijana Na
Wakinamama wengi zaidi wa Kitanzania.
Aliyasema hayo Jana
wakati alipokuwa akimuombea Kura mgombea Urais kwa tiketi ya chama Cha
mapinduzi John Magufuli ,mbunge wa Jimbo hilo Noah Lembrus pamoja na
mgombea udiwani wa kata ya Kiranyi Lorivi Muro mkutano uliofanyika
katika viwanja vya barazani Ngateu ,iliopo ndani ya halmashauri ya
Arusha Wilayani Arumeru mkoani Arusha.
Alibainisha kuwa ni
vyema wananchi wasirudie kufanya makosa waliyoyafanya katika uchaguzi
iliopita wa mwaka 2015 ambapo walimnyima Rais Kura pamoja na madiwani
,lakini pamoja na yote hayo Rais hakuwatupa bali aliweza kuwaletea
Maendeleo ikiwemo Mradi mkubwa wa maji wa zaidi ya bilioni 520 ,umeme
,zahanati pamoja na kuwa kutoa elimu bure kwa watoto wetu.
Alisema kuwa nivyema
wakafanya Maamuzi na kuchagua kiongozi ambaye ataweza atawaletea
Maendeleo ,atakae jali shida za wananchi ,atakaeweza kushirikiana na
wananchi na kupeleka shida zao bungeni ili ziweze kutatuliwa na Serikali
na sio kuchagua viongozi ambao wakiwatuma kuwawakilisha hawarudi kujua
changamoto zao bali wanasubiri kipindi Cha kampeni ndio wanarudi kupiga
kelele
Nae Mgombea ubunge
Jimbo la Arumeru Magharibi Noah Saputu ametumia fursa hiyo kuelezea
malengo yaliyoainishwa kwenye Ilani ya chama Cha mapinduzi kwa kipindi
Cha miaka mitano ijayo Na kuwaahidi kutekeleza yale yote aliyowaahidi
mara baada ya kushinda katika jimbo hilo.
Alisema anatambua
katika kata ya Kiranyi kuna changamoto kubwa ya ukosefu wa maji pamoja
na barabara ,ambapo alifafanua kuwa wakimpa ridhaa ya kuongoza Mambo
ambayo ataanza kuyashulikia ni maswala haya ili wananchi wa kata hiyo
waachane na kero hii.
Kwa upande wake
Mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Arusha Omary Lumato alisema kuwa Kama
wanapenda maendeleo, wanahamu ya maendeleo wachague timu ya watu ambao
wanaoweza kuwaleta maendeleo mazuri ambayo yataweza kufanya nchi yetu
kuwa Kama Ulaya
Aliwataka wananchi
wasifanye makosa maana magufuli ajawabagua japo katika kipindi
kilichopita walimnyima Kura Ila yeye kwakuwa Ni Rais wa wote amewapa
miradi mikubwa ya maji bilioni 520 ambayo kupitia fedha za halmashauri
wasingeweza kupata labda ipite miaka 143 ijayo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...