Na.Vero Ignatus,Longido

Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Longido Dkt.Jumaa Mhina amemtangaza mshindi wa Ubunge katika Jimbo hilo  Dkt.Steven Kiruswa,kwa ushindi wa kura 61,885 ,sawa na asilimia 97.5,huku bi Pauline Laizer(chadema ) akipata kura 1,037 sawa na asilimia 1.63 

Dkt.Mhina alisema kuwa waliojiandikisha kupiga kura katika Jimbo hilo kwa idadi yao ni 76,468, ambapo waliopiga kura ni waliopiga ni 63,008,NRA Feruz Juma kura 21 sawa na asilimia 0.3,CUF Abubakar Mukadam kura 65 sawa alimimia 0.5.

Dkt.Mhina alisema kuwa Jimbo hilo lina Jumla ya Kata 18 ambapo madiwani wote wa Chama cha Mapinduzi walipita bila kupinga .Aidha aliwashukuru wasimamizi wote wa uchaguzi,mawakala ,Jeshi la Polisi pamoja na wananchi wote wa Jimbo hilo kwa kupiga kura kwa Amani na utulivu ambapo Waliweza kumaliza salama.

Akizungumza Mara baada ya kutangaza mahindi wa Ubunge Jimbo la Longido kupitia CCM Dkt.Steven Lemon Kiruswa aliwashukuru wananchi kwa kumwamini na kumchagua tena na ameahidi kutekeleza yale yote aliyoyasema kipindi cha Kampeni 

Kiruswa alisema kuwa atashirikiana vyema na madiwani waliochaguliwa Ili kuhakikishakuwa wanapambania maendeleo ya wanalongido bila kujali itikadi zao na bila ubaguzi wowote

Kwa upande wake Mkazi wa Longido Seret Steven alisema kuwa, furaha yao wananchi wa Longido umetimia kwa kumpatia Dkt.Kirushwa ,kwani changamoto zao zote wamepata pa kusemwa na watapata utatuzi kikamilifu

Wakati huohuo Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Monduli Steven Ulaya   amemtangaza Fred Lowassa (CCM)kuwa mbunge wa Jimbo hilo kwa ushindi wa jumla ya kura 72,502 ,sawa na asilimia 93.23 ,huku mpizani wake sesilia Ndoss (Chadema )akipata kura 4637 sawa na asilimia 5.69


Mbunge wa Jimbo la Longido Steven Kirushwa akionyesha Certificate Mara baada ya kutangazwa rasmi mbunge wa Jimbo hilo
Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Longido Dkt.Jumaa Mhina akimtangaza mshindi wa Ubunge Jimbo La Longido Dkt.Steven Kiruswa



Baadhi ya wananchi waliojitokeza kumsikiliza matokeo ya kutangazwa mshindi katika Jimbo hilo.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...