Na Muhidin Amri,Tunduru,

UCHAGUZI wa madiwani,Ubunge na Urais  katika majimbo mawili ya uchaguzi ya Tunduru Kusini na Tunduru kaskazini mkoani Ruvuma umefanyika kwa amani na utulivu wa hali ya juu huku wananchi wakiipongeza Serikali kwa kuweka mazingira mazuri ya kupigia kura.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti,baadhi ya wananchi kutoka kijiji cha Muhesi kata ya Muhesi,Masonya na Mlingoti Mashariki  jimbo la Tunduru Kaskazini wamesema, mazinngira Rafiki yaliyokuwepo na ushawishi mkubwa  wa wagombea umehamasisha sana wananchi kujitokeza kuchagua viongozi wao.

Hata hivyo,wamewataka wagombea kukubali matokeo yatakayotangazwa na kutowashawishi wafuasi wao kufanya vurugu pindi itakapotokea wameshindwa katika uchaguzi huo.

Sulushi Mwarabu mkazi wa kijiji cha Muhesi ameipongeza Tume ya Taifa ya Uchaguzi(NEC)kwa kuaandaa vizuri uchaguzi mkuu wa mwaka huu ambao umetoa fursa kwa watu wengi kujitokeza katika vituo vya kupigia kura.

Mkazi mwingine Rajabu Athumani amesema, uchaguzi wa mwaka huu umefanyika vizuri tofauti na ilivyodhaniwa na baadhi ya watu kwamba  wananchi hawatajitokeza katika vituo vya kupigia kura.

Aliwaomba wananchi wenzake kuhakikisha mara watakapopiga kura kurudi majumbani, badala ya kukaa vituoni ili kuepuka kupata matatizo kutoka kwa vyombo vya ulinzi na usalama ambavyo viko makini katika kuimarisha ulinzi.

Sabina Lipukila alisema, mwaka huu vituo vya kupigia kura ni vingi tofauti na chaguzi zilizopita ambapo wananchi wanapofika katika vituo hawachukui muda mrefu na kuwepo kwa mazingira rafiki kwa makundi maalum ya walemavu,wajawazito na wanawake wenye  watoto wadogo kumechochea uchaguzi wa mwaka huu kuwa wa mfano.

Aidha alisema,  jambo linguine lililowafurahisha watu wengi ni pale serikali kupitia tume ya taifa ya uchaguzi kutoa kuweka utaratibu  wa kutumia  leseni ya udereva,kadi ya uraia na paspoti ya kusafiria  nayo imehamasisha sana wananchi kujitokeza kwa wingi katika uchaguzi wa mwaka huu.

Lipukila ameipongeza serikali kwa kufanya marekebisho makubwa katika sheria za uchaguzi ambayo siku za nyuma yalichangia baadhi ya watu kushindwa kupiga kura na kumpongeza mkurugenzi wa uchaguziwa wilaya ya Tunduru kusimamia vizuri uchaguzi wa mwaka huu kama kufunguliwa vituo vya kupigia kura kwa wakati.

Kwa upande wake,Mkurugenzi wa uchaguzi  wa  majimbo ya Tunduru Kaskazini na Kusini Gasper Balyomi alisema,maandalizi yote ya uchaguzi yamekamilika  na vituo vyote  540 vimefunguliwa mapema saa 1 asubuhi kama ilivyopangwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi.

Balyomi alisema,kama tume ya uchaguzi wamejipanga vema kuhakikisha kila mtu mwenye sifa anapata nafasi ya kwenda kupiga kura na tume itahakikisha  inatenda haki kwa kila chama na kila mgombea ikiwemo kutoa matokeo ya uchaguzi huo kwa wakati.

Hata hivyo,ameomba wapiga kura katika majimbo yote ya uchaguzi kutoa ushirikiano kwa tume na kuwaasa wale waliopiga kura kurudi nyumbani mara baada ya kupiga kura na kujiepusha na miemko ya kisiasa ambayo inaweza kuathiri zoezi zima la upigaji kura na hata kupata matatizo.

“namshukuru Mungu mpaka sasa hivi uchaguzi unaendelea vizuri na hakuna matatizo katika vituo vyote vya kupigia kura,naendelea kuwasihi wananchi mara baada ya kupiga kura ni vema warudi majumbani badala ya kukaa katika vituo kwani wapo watu waliopewa kazi hiyo”alisema Balyomi.

Picha,Baadhi ya wananchi wa kijiji cha Muhesi kata ya Muhesi waliojitokeza kupita kura wakiwa katika mstari kwa ajili ya kuingia katika chumba cha kupiga kura kuchagua diwani,mbunge na Rais katika uchaguzi Mkuu uliofanyika leo(jana)nchini kote ambapo  wameipongeza Serikali kupitia Tume ya Taifa ya Uchuaguzi kuweka mazingira mazuri na rafiki yaliyofanikisha uchaguzi mkuu wa mwaka huu.Picha na Muhidin Amri

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...