Mkurugenzi wa Kituo cha Life and Hope Sober House Bagamoyo, Al-Karim Bhanji (wa tatu kushoto) akipokea sehemu ya msaada wa vyakula na vitakasa mikono kutoka kwa Rais wa Mbezi Beach Rotary Club, Abel Mbilinyi katika hafla fupi iliyofanyika kituoni hapo, Bagamoyo mkoani, Pwani, jana.
Mkurugenzi wa Kituo cha Life and Hope Sober House Bagamoyo, Al-Karim Bhanji (kushoto) akipokea sehemu ya msaada wa vyakula na vitakasa mikono kutoka kwa Rais wa Mbezi Beach Rotary Club, Abel Mbilinyi katika hafla fupi iliyofanyika kituoni hapo, Bagamoyo mkoani, Pwani, jana.
  ASASI ya Rotary Club (Mbezi Beach) inayoshughulika na utoaji wa misaada kwa jamii imetoa msaada wa vyakula na vitakasa mikono kwa kituo cha  Life and Hope Sober House kinachowatunza warahibu wa dawa za kulevya huko Bagamoyo, Mkoani Pwani.

=====   ======   =====


Akizungumza wakati wa kukabidhi msaada huo Rais wa Mbezi Beach, Rotary Club Abel Mbilinyi amesema kuwa asasi hiyo imeendelea kuwa karibu na jamii kwa kutoa misaada katika njanya mbalimbali ikiwemo elimu, afya na hata majanga.

"Leo tunakabidhi misaada kwa kituo hiki ikiwa ni sehemu ya kushiriki kutatua changamoto kwa jamii, tunaamini hiki kidogo kitasaidia kuongeza pale palipopungua" amesema Mbilinyi.

Amesema, asasi hiyo imekuwa ikishirikiana na Serikali wakati na baada ya majanga katika kuhakikisha jamii inabaki salama wakati  wote.

"Katika ujenzi wa Taifa la viwanda lazima tuwaandae watoto katika masuala ya elimu na hata afya, hivyo tutaendelea kushirikiana na Serikali na wadau wengine wa maendeleo katika kuhakikisha azma hiyo inafikiwa"
Amesema.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Life and Hope Sober House Bagamoyo Al-Karim Bhanji ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa asasi ya Life and Hope Rehabilitation Organisation ameshukuru kwa msaada huo na kueleza kuwa kituo hicho kimeendelea kuwasaidia vijana walioingia katika utumiaji wa dawa za kulevya na kuwapa elimu, misaada ya kiafya na hatimaye kuwarudisha katika jamii ili waendelee na shughuli za kujenga taifa.

"Tunashukuru kwa msaada huu ambao umeelekezwa kuwa vijana tunaowahudumia, tunaomba na asasi nyingine ziendelee kujitokeza ili tuweze kuwahudumia na kuwaokoa vijana walioathirika na matumizi ya dawa za kulevya hatimaye waweze kurudi uraiani na kuendelea na shughuli za kujenga taifa." Amesema.

Vilevile ameishukuru Serikali kwa kuendelea kutambua mchango wa Sober Houses katika kujenga taifa imara la kesho, pia amesisitiza wazazi walete vijana wao Sober au Methadone Clinic.

Rotary ni mtandao wa kimataifa unaojumuisha majirani, marafiki, na viongozi wanaofanya kazi za kujitolea ili kutatua matatizo kwenye jamii. Kwa zaidi ya miaka 110, wanachama wa Rotary wamejitolea kwa hali na mali kutekeleza miradi endelevu kwenye sekta za elimu, afya, maji, kudumisha amani, afya ya mama na mtoto, na kukuza vipato duni. Rotary inaamini kwamba, kwa pamoja tunaweza kuwa na ulimwengu ambao watu wanaungana na kuchukua hatua kuleta mabadiliko ya kudumu - kote ulimwenguni, katika jamii zetu, na ndani yetu wenyewe. Ulimwenguni kote kuna wanachama wa Rotary milioni 1.2.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...