Mkuu wa kitengo cha Mauzo, Usambazaji, Maduka na Huduma kwa wateja Vodacom Tanzania PLC, George Lugata (kulia) akielezea uwezo wa simu ya smart kitochi ambayo alikabidhiwa mteja, Jovith Muhandiki aliyezawadiwa kwa kutumia mtandao huo kwa muda wa miaka 20, hii ikiwa ni sehemu ya uzinduzi wa duka la kampuni hiyo lililopo jengo la Palm Village Mikocheni jijini Dar es Salaam. Katikati ni Mkurugenzi wa Biashara wa kampuni hiyo, Linda Riwa.
Mkurugenzi wa Biashara wa kampuni ya Vodacom Tanzania PLC, Linda Riwa na Msimamizi wa duka la Vodacom lililopo jengo la Palm Village Mikocheni, Atilio Lupala wakikata utepe kuzindua duka hilo jipya la kisasa
Mchumi wa jiji la Dodoma, aliyemwakilisha Mkurugenzi wa Jiji hilo, Charles Rwaembe (katikati) akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa duka la Vodacom lililoko eneo la Chang'ombe Jijini Dodoma. Wengine katika picha kulia ni Mkuu wa Mauzo Kanda ya kati Vodacom Tanzania PLC ,Grace Chambua na kushoto ni Meneja Mauzo Mwandamizi wa Vodacom Tanzania PLC kanda hiyo, Andrew Temu.
Baadhi ya Wafanyakazi wa Vodacom Tanzani PLC Kanda ya kati, wakifurahia baada ya kuzinduliwa duka jipya eneo la Chang'ombe Jijini Dodoma .
Baadhi ya wakazi wa eneo la Chang'ombe Jijini Dodoma wakiwa nje ya duka jipya la Vodacom wakishuhudia uzinduzi rasmi wa duka hilo jipya 
Mkuu wa Mauzo, Vodacom Tanzania PLC, Kanda ya Kati, Grace Chambua (kulia) akimkabidhi zawadi Eliudy Nghwali kama mteja aliyedumu ndani ya mtandao huo kwa miaka 20, kampuni hiyo inasherehekea miaka 20 tangu kuanzishwa kwake nchini. Anayeshuhudia katikati ni Meneja Mauzo Mwandamizi wa Vodacom Tanzania Kanda ya kati, Andrew Temu ,

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...