Mara baada ya kupoteza mchezo wa mzunguko wa
tano dhidi ya Polisi Tanzania, Kocha wa Timu ya Manispaa ya Kinondoni
KMC FC Habibu Kondo amesema kuwa bado anakiamini kikosi hicho kutokana
na uwezo waliokuwa nao wachezaji wake.
Kocha Habibu ametoa kauli hiyo leo wakati Timu
ya KMC FC ilipokuwa ikifanya mazoezi kwa ajili ya kujiandaa na mchezo
unaofuata dhidi ya Cost Union mchezo utakaopigwa Oktoba 14 Katika Uwanja
wa Uhuru Jijini Dar es Salaam.
Kocha Habibu amesema
kuwa kupitia mazoezi hayo timu hiyo inajiandaa kikamilifu katika
kujiweka tayari dhidi ya mchezo huo na kwamba makosa yaliyofanywa na
wachezaji hao katika mchezo uliopita yanafanyiwa kazi.
Habibu amefafanua
kuwa anakiamini kikosi hicho kwakuwa kinauwezo mzuri kikubwa kwasasa ni
kuendelea kujenga utulivu kwenye nafasi za kumalizia ili kupata matokeo
mazuri katika mchezo huo unaofuata.
“Timu inatengeneza
nafasi nzuri kwenye michezo lakini kwenye umaliziaji inakuwa
changamoto, kupitia mazoezi haya tunakwenda kukisuka kikosi chetu ili
kwenye michezo ijayo tupate matokeo ambayo awali tulikuwa tukiyapata”
amesema Kocha Habibu.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...