MGOMBEA urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi(CCM) Dk.John Magufuli akimnadi Askofu Josephat Gwajima

Na Said Mwishehe,Michuzi TV
MGOMBEA
urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi(CCM) Dk.John Magufuli amewapa
pole wananchi wa Jimbo la Kawe kutokana na kuchelewa kwa maendeleo
kutokana na kuwa na mbunge wa upinzani ambaye kwa kipindi cha miaka
mitano ameshindwa kuwapigania na kuwatetea kimaendeleo.
Hivyo
amewaaambia katika Uchaguzi Mkuu mwaka huu wahakikishe wanamchagua
mgombea ubunge wa CCM Askofu Joseph Gwajima ili ashirikiane naye kuleta
maendeleo ya wananchi wa Kawe.
Akizungunza
mbele ya wananchi wa Jimbo la Kawe na Kinondoni leo Oktoba 14 mwaka huu
, Dk.Magufuli pamoja na mambo mengine ametumia nafasi hiyo kueleza
anawapa pole wananchi wa Kawe.
"Poleni
Kawe,mmechelewa sana , miaka mitano nilikuja kuomba kura, na kwanafasi
ya ubunge kulikuwa na mtoto wa Sinde Warioba, mimi mlinipa lakini
mbunge hamkunipa, nilileta maendeleo, nilitegemea mbunge wenu (Halima
Mdee)atawatetea wana Kawe lakini hakufanya hivyo, hata nilipouliza
mawaziri kama anawasumbua kukumbusha maendeleo ya Kawe nimaambiwa hasemi
chochote.
"Hata hizi
barabara ambazo tumejenga Kawe tumetumia nguvu kubwa sana.Mradi wa
kuendeleza Jiji la Dar es Salaam DMDP Kinondoni,Ilala,Temeke,
Ukonga,Kigamboni wali pat miradi mingi lakini kwaa Kawe haikuwa hivyo
kwasababu hakuna wa kuiomba.Mbunge wa hapa Kawe akienda Bungeni anatoka
nje na wakati mwingine anafunga mdomo sasa unaombaje miradi
"Nimekuwa
Mbunge kwa miaka 20,nimekuwa Waziri kwa miaka 20, lazima mbunge ujenge
mahusiano na mawaziri. Kawe haina hospitali ya kufanya operesheni,
wakati Kigamboni wilaya mpya kuna hospitali mbili.Kawe hamjakosea Mungu
ila mlikosea kuchagua, mwaka huu Kawe fanyeni mabadiliko, nileteeni
Gwajima tulete mabadiliko, najua kuna kampeni chafu zinaendekea za
udini, na mitandaoni kuna fitina zinaendelea, leo hii wanasema Gwajima
ni Askofu ,wanaingiza udini,
"Mimimwenyewe
nilitakiwa niwe Padri nikashindwa, aani nikae bila kuoa wakati mama
Janeth yupo.Mimi ni Mkristo lakini jana nimeenda kuangalia maendeleo ya
ujenzi wa Msikiti pale Kinondoni, ambao niliuomba kwa Mfalme, wakati
namuomba Mfalme huo msikiti alishangaa akaniuliza dini gani nikamwambia
ni Mkristo.
"Kule
Chamwino nimechangisha Wakristo kwa ajili ya kujenga msikiti mzuri wa
kisasa tena wa ghorofa ambao utakuwa unaingiza waumini i 500, hiyo ndio
Tanzania tuliyonayo na tuliyoachiwa na waasisi wa Taifa hili. Tanzania
ambayo imeendelea watu wanaleta udini?
"Makabila
yote yapo hapa mkutanoni na wakati leotunaadhimisha miaka 21 ya
kukumbuka kifo cha .walimu Nyerere aliyepinga udini na ukabila halafu
wanakuja watu wa kuanza kuleta udini,"amesema Dk.Magufuli wakati
akimuombea kura Askofu Gwajima.
Amewaambia
wananchi hao kwamba wakati akiwa Waziri ameshiriki kupima viwanja Kawe
na kuongeza Kawe kubwa na wala haistahili kuwa hivyo ilivyo sasa.Hivyo
amewaomba wampelekee Gwajima. "Nileteeni Gwajima, nileteeni
Gwajima,mtaleta? Nina machungu na Kawe,miaka mitano imepita sijafanya
mambo makubwa Kawe, nataka kuleta maendeleo ya Kawe, katika miaka mitano
ya urais wangu naomba mniletee Gwajima.
"Na
baada ya Gwajima kuchaguliwa kaa na watu hawa ili uwasikilize shida
zao, ukae na akina mama na walemavu wapate mikopo inayotolewa na
serikali, wapiganie wananchi masikini.Kuna eneo la bandari ya Mbweni
,kwani bandari nayo ni kero, watu kufanyabiashara pale ni dhambi, yaani
wa Mbagala aende bandari ya Dar es Salaam halafu wa Kawe washindwe. Tena
ngoja wakuchague ile bandari nitakupa na fedha za kuiendeleza.
"Sitaki
kusema uongo,mbele ya viongozi wa dini,nataka siku nikifa nikafagie
hata chumba cha Malaika, naomba mniletee.Gwajima hakuongoza ,
aliyeongoza ni mtoto wa dada angu anaitwa Furaha, dada yangu Asteria,
kama kumleta ningemleta mtoto wa dada yangu.Akatae kama Furaha sio mtoto
wa dada yangu.
"Wa pili
Kiiziga ambaye amewahi kuwa Mbunge wa Bunge la Afrika Masharili, sio
kwamba hawafai lakini Gwagima amewazidi.Kazi ya ubunge inahitaji mtu
jasiri,asiyeogopa, ana hofu ya Mungu, Kamati Kuu imeona Gwajima ndio
anafaa kuwa Mbunge wa Kawe.
"Wangapi
wataniletea Gwajima? , nileteeni Gwajima,Kawe hakuna viwanda
vingi,mnadhambi gani, mmmebaki na kiwanda cha Wazo tu, tuna mipango ya
kujenga viwanda kwanini kusiwe na viwanda Kawe, nipeni Gwajima tujenge
viwanda,"amesema Dk.Magufuli.
Kwa
upande wa Kinondoni, Dk.Magufuli amewaba wananchi wa jimbo hilo
kuhakikisha wanamchagu mgombea ubunge Abass Tarima kwani anamfahamu
vizuri na maisha yake yamekuwa Kinondoni."Nafahamu kuna changamoto ya
mafuriko Kiinondoni ,tumepanga kutatua kero hiyo kwa kuujenga mto
ng'ombe, hata hivyo baadhi ya mafuriko yanatokana na wananchi wenyewe."
Akimzungumzia
zaidi Dk.Magufuli amewapa siri Tarimba alifiwa na watoto wake wawili
ambao alikuwa anawategemea ,mmoja ruban na mwingine injinia na wote
walikufa ndani ya wiki moja."Nlipoenda kumpa pole na siku hiyo bado
alikuwa anazubgumzia maendeleo ya Kinondoni, na nilimwambia nitatamani
siku moja kama atagombea ubunge,Mungu akasikia na Tarimba akaongoza kura
za maoni.
"Kama
Kinondoni mnataka kulete mabadiliko ya kweli naomba mniletee Tarimba, ni
mtu wa pekee.Hata hivyo wagombea wetu kila mmoja anahistoria
yake.Mgombea ubunge Ukonga Jeru Silaa baba yake alikufa wakati
ananifanyia kampeni mwaka 2015, kijana wa watu alitulia, mwaka 2015
alikosa lakini tumemleta tena Ukonga naomba mniletee Jery silaa.Kila
mgombea ana sifa yake hapa,"amefafanua Dk.Magufuli.
Mbali
ya kuwazungumzia wagombea hao,Dk.Magufuli.amewaomba wananchi kuendelea
kuwa wamoja na kuwataka wajiepishe na wagombea ambao wanachochea vurugu
kwani mgombea urais mmoja wa tayari ameshakata tiketi ya ndege na
uchaguzi ukishamalizika na kusababisha machafuko anaondoka.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...