Na Shukrani Kawogo, Njombe.
Mbunge mteule wa jimbo la Ludwa Mkoani Njombe Joseph Kamonga amewaahidi wakazi wa kata ya Manda, Ruhuhu na Iwela kuboresha miundombinu ya barabara, maji, kuongeza walimu mashuleni pamoja na kufuatilia kwa karibu uanzishwaji wa bandari ya manda ili iweze kuwanufaisha wananchi.
Hayo ameyasema alipofanya mikutano ya hadhara katika vijiji hivyo ikiwa ni muendelezo wa kampeni ya kumuombea kura Rais John Magufuli, madiwani pamoja na kujua changamoto mbalimbali zinazowakabili wananchi.
Ameongeza kuwa wakazi wa maeneo hayo wamekuwa wakipatwa na changamoto mbalimbali hasa ya maji ambapo tayari wameanza kufanya ufumbuzi wa haraka kwa kuchimba visima huku wakiendelea na mpango wa muda mrefu wa kuiomba serikali kutuma wataalamu kuja katika ziwa nyasa na kuyafanyia utafiti wa maji ya ziwa hilo ili yaweze kuvutwa na kupelekwa kwa ajili ya matumizi ya wananchi.
Amesema kuwa sanjari na mpango huo wa kuleta watafiti pia kuna mradi wa maji ambao utaanzia Lifua mpaka Manda kitu ambacho kitamaliza changamoto hiyo ya maji.
Vile vile amewaomba wananchi kumchagua rais John Mgufuli ili aweze kumalizia bandari ya Manda ambayo itawasaidia wananchi hao kupata fursa mbalimbali ambazo zitawaletea maendeleo katika maeneo hayo.
“Wananchi mnapaswa kuchagua wagombea wa CCM ili tuweze kuwaletea maendeleo kwa urahisi zaidi kwani bandari hiyo itakapokamilika itawasaidia vijana kupata fursa mbalimbali ikiwemo kusafirisha abiria wanaoshuka kwenye meli na kuwapeleka katika maeneo mbalimbali”, Alisema Kamonga.
Aidha katika suala la uhaba wa walimu mbunge huyo amesema kuwa ili maendeleo ya Ludewa yaweze kukua kwa kasi kunahitajika watoto wetu kupata elimu hivyo watahakikisha wanatafuta walimu ambao watasaidia kusukuma maendeleo ya wanafunzi.
Katika ziara hiyo mbunge huyo ameambatana na Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi wa wilaya ya Ludewa Stanley Kolimba, Katibu wa CCM wilaya Bakari Mfaume pamoja na wajumbe wa kamati ya siasa ambao wanatarajia kuzunguka katika vijiji 66 vilivyopo katika kata 26 na mpaka sasa tayari wameshapita katika vijiji 9 kati ya vijiji hivyo
Mbunge mteule Joseph Kamonga (kulia) akiwa ameambatana na diwani wa kata ya Manda Efrida Kilumbo ( aliyeshika kipaza sauti) pamoja na wajumbe wa kamati ya kampeni wakiwa waamepiga magoti kumuombea kura Rais John Magufuli pamoja na diwani wa kata ya Manda Efrida Kilumbo
Mbunge mteule wa Jimbo la Ludewa Joseph Kamonga akiwa ameshika maji aliyokabidhiwa na wananchi wa Kijiji Cha Mbongo kisaula ambayo alikabidhiwa kwa lengo la kumuonyesha aina ya maji wanayotumia.
Mbunge mteule Joseph Kamonga akiongea na wananchi ambao walisimamisha msafara wake njiani ili kumsalimia wakati akielekea Manda.
Mbunge mteule Joseph Kamonga, akiingia eneo la mkutano huku akiwa ameongozana na wananchi ambao wametoka kumpokea
Katibu wa CCM wilaya ya Ludewa Bakari Mfaume akiongea na wananchi juu ya maendeleo katika Kijiji Cha Sagalu kilichopo kata ya Manda wilayani humo.
Mbunge mteule Joseph Kamonga akiongea na wananchi wa Kijiji Cha makata kilichopo kata ya Iwela wilayani Ludewa.
Katibu wa CCM wilaya Bakari Mfaume (kushoto)akizungumza jambo na mgombea udiwani wa kata ya Manda Efrida Kilumbo.
Mwenyekiti wa CCM wilaya Stainley Kolimba akiwa amesimama na mgombea udiwani wa kata ya Iwela katika mkutano uliofanyika katika Kijiji Cha Makata.
Mwenyekiti wa CCM wilaya Stainley Kolimba kushoto akiteta jambo na mbunge mteule Joseph Kamonga pamoja na mgombea udiwani wa kata ya Manda Efrida Kilumbo kabla ya mkutano kuanza katika Kijiji cha Mbongo kisaula kilichopo katika kata hiyo wilayani Ludewa.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...