Na,Jusline Marco
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Iddy Hassan Kimanta amesema kuwa sekta ya kilimo ni mwajiri wa zaidi ya asilimia 60 ya watanzania huchangia asilimia 29.1 ya pato la taifa huku ssilimia 30 ya pato la taifa linatolana na uuzaji wa bidhaa nje ya nchini na asilimia 65 ya malighafi za viwanda vya ndani .
Akifungua kikao kazi cha jukwaa la wawekezaji katika utengezaji wa mbolea na visaidizi vyake nchini,kikao kilichofanyika jijini Arusha ambapo amewataka wakulima kuwatumia wataalamu wa kilimo ili waweze kuzalisha kwa tija huku akiwataka pia wadau mbalimbali wa maendeleo,maafisa ugani pamoja na watafiti kuendelea kutoa elimu ya matumizi sahihi ya mbolea na pembejeo kwa wakulima nchini.
"Kumekuwa na dhana potofu zinazosambazwa kwamba mbolea ni sumu inayoharibu ardhi kqa kuifanya iwe tegemezi kwa mbolea za viwandani,dhana hiyo potofu nimekuwa kikwazo kikubwa sana kwa wakulima kutumia mbolea hivyo kuwa kilwazo kwa wawekezaji".Alisema Kimanta
Pamoja na hayo Kimanta amesema bado kuna changamoto ya uelewa kwa wakulima kuhusu matumizi sahihi ya visaidizi vya mbolea psmoja na mbolea zinazozalishwa ndani ya nchi kuonekana hazina ubora ikilinganishwa na mbolea zinazotoka nje ya nchi.
Amesema kuwa nchi ya Tanzania kuishi kwa kutegemea mbolea kutoka nje kwa zaidi ya asilimia 90 ni hatari kwa nchi ambapo amesema kuwa bado viwanda vya mbolea na visaidizi vyake hapa nchini vinategeneza asilimia 6 tu ya mahitaji ya wakulima,ambapo amewataka wakulima kuzingatia kilimo cha umwagiliaji,kufuata kanuni bora za kilimo wanazoelekezwa na maafisa ugani,matumizi sahihi ya pembejeo za kilimo ikiwemo mbolea,visaidizi vya mbolea na madawa ili luongeza uzalishaji na tija katika kilimo.
Pamoja na hayo Mkuu huyo wa Mkoa ameagiza kikosi kazi hicho kiwe ni uzundizi wa mkakati wa kudumu wa kutafuta namna ya kuondoa changanoto za uwekezaji katika tasnia ya mbolea ili nchi ya Tanzania ijitosheleze katika mahitaji ya ndani na zaidi ya kuuza nje ya nchi,kuimarisha mahusiano na taasisi ya utafiti wa kilimo TARI ili kuweza kuelewa aina sahihi za mbolea za kutengeneza kwa kila zao na kwa aina ya udongo pamoja na maafisa kilimi wa mkoa wa Arusha kushirikiana na Mrajis Msaidizi wa vyama vya ushirika wa mkoa kuhamasisha wakulima kujiunga ili kununua mbolea zinazotengenezwa na viwanda vya tanzania badala ya kutegemea mbolea za kuagiza kutoka nje ya nchi.
Awali akizungumza katika kikao kazi hicho Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi wa TFRA Prof.Anthony Manoni Mshandete amesema kuwa kikao hicho kimelenga kujadili kwa pamoja namna bora ya kutatua changamoto zinazoikabili tasnia ya mbolea nchini.
Aidha ameeleza kuwa kutokana na changamoto zilizoikabili tasnia ya mbolea nchini,Tanzania inategemea mbolea za kuagiza kutoka nje ya nchi kwa zaidi ya asilimia 90 huku asilimia 10 zikizalishwa hapa nchini ambapo ameeleza kuwa utegemezi wa mbolea za nje ni hatari kwa usalama wa nchi kwasababu pakitokea mbolea hizo kutoingia nchini basibTanzania itaingia kwenye baa la njaa.
Ameongeza kuwa kutokana na ugonjwa COVID 19 kuanza duniani umeathiri kwa kiasi kikuwa baadhi ya biashara ikiwemo uzalishaji viwandani hali iliyopelekea kupanda kwa bei ya mbolea kwenye soko la dunia ambapo mwezi juni mwaka huu bei ya mbolea ya kupandia(UREA) na ya kukuzia (DAP)zimepanda kutoka wastani wa dolla za kimarekani 240 na 291 hadi kufikia dolla 260 na 355.
"Ongezeko hilo ni kubwa ukilinganisha na ongezeko la bei za mbolea duniani ndani ya miezi mitatu iliyopita hivyo ni wazi kwamba kasi ya ongezeko la bei za mbolea duniani limechochewa na COVID 19,kwa vile ugonjwa huo bado haujapatiwa tiba wala chanjo ni wazi kwamba kuna uwezekano mkubwa wa bei za mbolea kuendelea kuongezeka."alisema Prof.Anthony
Vilevile ameeleza kuwa kwa kuona changamoto zilizoikabili tasnia ya mbolea ikiwemo uingizwaji wa mbolea bandia nchini,mbolea kuchelewa kuwafikia wakulima na bei kubwa ya mbolea zilizoingia nchini kutoka nje ambapo Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lilitunga sheria ya mbolea namba 9 ya mwaka 2009 mnamo mwaka 2011 ili kusimamia ubora wa mbolea katika mnyororo wa thamani kuanzia utengenezaji,uingizaji ndani ya nchi,usambazaji,utunzaji,na uuzaji ndani na nje ya nchi.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe.Iddy Hassan Kimanta akizungumza katika ufunguzi wa kikaokazi cha Jukwaa la wawekezaji katika utengenezaji wa mbolea na visaidizi vyake nchini,kikao kilichofanyika jijini Arusha.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...