NA BALTAZAR MASHAKA, MWANZA
 
MENEJA kampeni wa mgombea ubunge wa CCM Jimbo la Sengerema, Deogratius Medard (42), mkazi wa Kata ya  Ibisabageni ktika Wilaya ya Sengerema,amefariki dunia akidaiwa  kula chakula kinachosadikiwa kuwa na sumu.

Marehemu huyo alikuwa meneja kampeni wa mgombea ubunge wa CCM, Hamis Mwagao Tabasamu,alifariki dunia ghafla kabla ya kupatiwa matibabu kwenye Hospitali Teule ya Wilaya ya Sengerema.

Akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na kifo cha Medard, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Jumanne Muliro alisema, tukio hilo lilitokea majira ya saa 12:35 jioni katika Hospitali Teule ya Wilaya ya Sengerema kuwa mtu mmoja Deograrius Medard alifariki dunia.

Alisema marehemu ambaye ni meneja kampeni wa mgombea wa CCM kwnye Jimbo la Sengerema Hamis Mwagao Tabasamu, kabla ya kufikwa na mauti alilalamika kuumwa tumbo baada ya kula chakula (makandekwa chai) na akalamika kukimbizwa hospitali lakini apoteza maisha kabla ya kupata tiba.

Muliro alisema kuwa jeshi hilo linaendelea na uchunguzi ili kubaini chanzo cha kifo hicho kama kimesababishwa na sumu na ni sumu aina gani.

Mbali na uchunguzi pia linaendelea na mahoajino na watu kadhaa waliokuwa na marehemu Medard kwenye kampeni kabla ya kifo ili kubaini chanzo halisi cha kilichosababisha meneja kampeni huyo wa mgombea wa CCM.

Aidha jeshi hilo mkoani humu limesema limejipanga vizuri kuelekea uchaguzi mkuu na kuwataka wananchi wajitokeze kupiga kura Oktoba 28, bila hofu.

Kamanda huyo wa polisi alisema kampeni zinaendelea vizuri na hkuna matukio makubwa ya kutisha yaliyotokea mkoani Mwanza kwani jeshi hilo limejipanga kuhakikisha amani na utulivu unakuwepo muda wote ili kuwawezesha wananchi kupiga kura.

Alisema jeshi hilo halitamvumilia mtu au kikundi chochote chenye mipango ya kufanya vitendo vya uvunjifu wa amani kwenye mchakato huo wa uchaguzi mkuu wa 2020 na watakaothubutu watashughuliwa kwa mujibu wa kisheria.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Jumanne Muliro akitoa taarifa za matukio ya uhalifu kwa waandishi wa hbari jana likiwemo tukio la kifo cha meneja kampeni wa mgombea ubunge jimbo la Sengerema.Picha Baltazar Mashaka
………………………………………………………………………….

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...