Yassir Simba, Michuzi TV

Raundi ya Saba ya ligi kuu Tanzania bara VPL imeendelea tena Oktoba 22,2020 katika dimba la Uhuru jijini Dar es Salaam ikiwakutanisha timu ya Yanga dhidi ya maafande wa Jeshi la Polisi Tanzania kutoka mkoani Kilimanjaro.

Mchezo huo uliopigwa majira ya saa kumi kamili jioni ikimshuhudia kocha mpya wa klabu ya Yanga akianza kibarua chake cha kwanza katika klabu hiyo kwa ushindi wa bao moja kwa sifuri dhidi ya Polisi Tanzania.

Mchezo huo uliotawaliwa na matumizi ya mbinu zaidi huku Polisi Tanzania wakitawala mchezo kwa kiasi chake huku Yanga wakiwa nyumbani wakihangaika kupata matokeo ili  kukimbizana na mwendo wa kusaka ubingwa wa ligi kuu Tanzania Bara VPL msimu huu.

Timu zote mbili zilitengeneza nafasi katika nyakati tofauti huku Feisal Salum akipiga mashuti matatu yaliyopanguliwa na mlinda mlango Manyika Junior wa Polisi Tanzania aliyekuwa katika kiwango bora sana Kwenye mchezo huo, iliwachukua Yanga dakika sabini za mchezo kupata bao la utangulizi na la ushindi katika mchezo huo ambapo Mukoko Tonombe akimalizia kazi nzuri iliyofanywa na Farid Mussa kwa shuti kali ndani ya kumi na nane liliyomshinda mlinda mlango wa Polisi Tanzania Manyika Junior nakutinga wavuni.

Kutokana na matokeo hayo rasmi Yanga anasogea nafasi moja juu mpaka nafasi nafasi ya pili ya msimamo wa ligi Kuu Tanzania bara VPL akicheza michezo sita na kujikusanyia alama kumi na sita huku mtani wake wa jadi Simba Sports Klabu akishuka hadi nafasi ya tatu katika msimamo wa ligi mara baada ya kupoteza mchezo dhidi ya Prisons katika uwanja wa Nelson Mandela mjini Sumbawanga.









 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...