Kampeni meneja wa mgombea ubunge mteule jimbo la
Singida Kaskazini, Elia Digha(wa kwanza kushoto) akijadiliana
jambo na katibu wa Hamasa Mkoa wa Singida wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika kijiji cha Kinyamwambo, Kata ya Merya.

 Kampeni meneja msaidizi, Shabani Limu(wa kwanza kushoto)
 akipokea maelekezo kutoka kwa kampeni meneja wa mgombea
ubunge mteule wa jimbo la Singida Kaskazini, Ramadhani Ighondo wakati wa kampeni hizo.
 Mgombea ubunge mteule wa jimbo la Singida Kaskazini, Ramadhani Ighondo akinadi sera za ccm pamoja na kuomba kura kwa wananchi ili aweze kuwa mbunge wa jimbo hilo.

 Mgombea ubunge jimbo la Singida Kaskazini, Ramadhani
Ighondo(wa kwanza kulia akiwatambulisha pamoja na kuwaombea kura
wagombea udiwani wateule wa jimbo la Singida Kaskazini (Picha zote na
Jumbe Ismailly.)


Na Jumbe Ismailly, Singida

MGOMBEA Ubunge mteule wa jimbo la Singida Kaskazini, Ramadhani Ighondo
ameahidi kwamba endapo atafanikiwa kupata ridhaa na kuwa mbunge wa
jimbo hilo atahakikisha soko la uhakika la kuuza mazao ya wakulima wa
jimbo hilo linapatikana na hivyo kuwapunguzia wakulima gharama za
usafirishaji.

Ighondo ametoa ahadi hiyo kwenye mkutano wa kampeni za uchaguzi
uliofanyika katika Kijiji cha Kinyamwambo, Kata ya Merya,wilayani 
Singida vijijini alipokuwa akiomba kura za kuchaguliwa kuwa mbunge wa
jimbo hilo.

“Mimi nataka hiv...i tuanzishe soko letu la uhakika la mazao la Wilaya
ili tuweze kuwa na sauti ya kuuza mazao yetu kwenye soko letu lililopo
katika Wilaya yetu na tuweze kuwa na uwezo wa kuamua bei ya masoko ya
mazao yetu”amesisitiza huku akishangiliwa na wananchi waliohudhuria
mkutano huo.

Aidha mgombea huyo mteule amefafanua kwamba endapo soko hilo la
uhakika la kuuza mazao yao litakuwepo watakuwa na sauti pia ya kuamua
mazao yao wayauze kwa bei gani badala ya kuendelea kulitegemea soko la
kimataifa la zao la vitunguu lililopo Manispaa ya Singida,linalotawaliwa na wingi wa madalali ambao huwakwamisha wakulima hao kuuza mazao yao kwa bei waitakayo.

Kwa mujibu wa Ighondo amesema kuwa, haiwezekani wakulima wateseke kuanzia hatua ya kupanda mbegu wakati madalali wa mjini Singida wakijiandaa kushona suti tayari kwa ajili ya kupokea vitunguu kutoka kwa wakulima ambao hawana sauti na bei ya soko ya wakati huo.

“Wakati wewe mkulima unanza kupanda mbegu za vitunguu mwenzako anaanza kushona tai,ukianza kufukua vitunguu,dalali anaanza kupiga pasi sutiyake halafu ukienda kukutana naye sokoni anakupiga bei,anakupiga zaidi ya hali halisi ya kipimo cha kitunguu kilivyo.”amesema.

Hata hivyo mgombea huyo ameahidi  kuboresha miundombinu ya barabara
ili kuhakikisha inakuwa ikipitika kwa kipindi cha mwaka mzima na
kuwapunguzia kero ya kusafirisha mazao yao kwa gharama kubwa kutokana
na barabara kukatika baada ya mvua kuanza kunyesha.

Akiwanadi wagombea wateule wa ubunge na udiwani wa jimbo la Singida
kaskazini, Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Singida vijijini Wiliamu
Nyalandu amesisitiza kwamba chama hicho kinasikitishwa na kauli
zinazotolewa na mgombea ubunge mteule wa jimbo hilo kupitia chama
kimoja cha siasa kwamba yeye bado hajahama CCM kwani bado hajarudisha
kadi wala sare za chama hicho.

“Udanganyifu wa kwanza unaoendelea na wale wanaogombea kupitia vyama
vingine,mimi sisemi mtu ila ujumbe utakuwa umefika,la kwanza mtu
anasema yeye bado hajahama ccm kwa sababu kadi yake ya ccm bado
hajairudisha na sare za ccm bado anazo.”ameeleza. 

Kwa upande wake meneja kampeni wa mgombea ubunge mteule wa jimbo
hilo, Elia Digha amesema pamoja na udogo wa Kijiji cha
Kinyamwambo,lakini mapema kabisa serikali ilikipatia huduma ya
niashati ya umeme pamoja na kuondoa changamoto ya upungufu wa madawati kwa kuwapatia madawati ya kutosha.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...