NA VICTOR MASANGU, KIBAHA
MWANADADA Sarah Zacharia (23) mkazi wa kwa
Mathiasi Wilayani Kibaha Mkoa wa Pwani ameibuka kidedea baada ya
kulitwaa taji la kumsaka miss Kiteshe 2020 huku nafasi ya mshindi wa
pili ikienda kwa Zadia Ally (19) na nafasi ya tatu
ikinyakuliwa na Zenat Rajab.
Kutokana na ushindi huo washindi hao watatu wamepata zawadi mbali
mbali kutoka kwa uongozi wa kiteshe pub sambamba na kuchaguliwa rasmi
kuwa mabalozi ambao watakuwa na jukumu la kutangaza mbuga ya
Nyerere National park iliyopo Wilayani Rufiji pamoja na vivutio mbali
mbali vinavyopatakanika katika eneo hilo.
Katika kinyan’ganyiro cha shindano hilo ambalo lilifanyika mwishoni
mwa wiki liliandaliwa kwa dhumuni la kuwasaka walimbwende
watatu ambao watakuwa na jukumu kubwa la kushirikiana na wadau wengine
pamoja na Serikali katika kuleta mabadiliko ya kutangaza utalii wa
ndani unaopatikana katika baadhi ya maeneo katika Mkoa wa Pwani.
Pia katika shindano hilo warembo hao waliweza kuulizwa maswali mbali
mbali na majaji yanayohusiana na masuala mbali mbali ya utalii pamoja
na mambo mengine ya kijamii ili kuweza kuona upeo wao katika sekta ya
utalii.
Kwa upande wake Miss Kiteshe Sarah Zacharia ambaye ametwaa taji hilo
amesema kwamba baada ya kuunyakua ushindi huo lengo lake kubwa ni
kuhakikisha anajipanga vilivyo katika kuleta mabadiliko katika
kutangaza utalii wa ndani ikiwemo pamoja na kutoa fursa kwa jamii kwa
kuwaelimisha umuhimu wa kutembelea mbuga mbali mbali za wanyama
ikiwemo ya Nyerere National Park.
“Kwanza kabisa napenda kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kuweza
kunifikisha hapa mpaka nimeweza kuchaguliwa kuwa miss kiteshe kwa
mwaka huu wa 2020 lakini ndoto yangu kubwa ambayo ninayo ni
kufika mbali zaidi ya hapa katika kutangaza mambo mbalimbali ya utalii wa ndani ukizingatia tuna mbuga nyingi ikiwemo ile ya
Nyerere National Park,”amesema Sarah.
Pi ametoa wito kwa washiriki wenzake ambao hawakuweza kupata nafasi ya
kuibuka kuwa washindi kutokata tamaa na badala yake wahakikishe
wanaendeleza vipaji vyao na fani ya kutangaza utalii wa ndani kupitia
fani ya ulimbwende pamoja na kushirikiana vilivyo na wadau wengine ili
kutimiza malengo waliyojiwekea.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...