Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme akizungumza kwenye Ibada kanisa la Anglikana la St.Nichalus mjini Songea.

Baadhi ya waumini wakifuatlia Ibada katika Kanisa la Anglikana la St.Nicholous mjini Songea.



Picha ya pamoja Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma na baadhi ya waumini na viongozi wa kanisa la Anglikana la St.Nichoulous mjini Songea.

……………………………………………………………………………………..

Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme ametoa rai kwa waumini kuendelea kuliombea Taifa hasa katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi Mkuu ili uweze kufanyika kwa amani na utulivu.

Mndeme ametoa rai Jumapili hii aliposhiriki Ibada na waumini wa Kanisa Anglikana Mtakatifu Nicholaus lililopo mjini Songea.

Mkuu wa Mkoa ambaye pia amechangia Ujenzi wa Nyumba ya Mchungaji saruji tani tatu yenye thamani ya zaidi ya shilingi 900,000,amewashukuru waumini wote kwa kuliombea Taifa la Tanzania kuanzia kipindi cha corona na hata kipindi hiki cha kuelekea Uchaguzi Mkuu ambao unatarajia kufanyika Oktoba 28 mwaka huu.

“Ndugu zangu nianze kuwashukuru kwa maombi yenu mnayoliombea Taifa hili,mkimuombea Rais wetu, mkiwaombea Mawaziri na viongozi wote wenye mamlaka katika nchi hii tunawashukuru sana maombi yenu yameifanya nchi yetu kuendelea kuwa na amani’’,alisema.

Hata hivyo Mndeme amesema umebaki muda mchache kuelekea Uchaguzi Mkuu hivyo amewaomba waumini kuendelea kuliombea Taifa la Tanzania ili Mwenyezi Mungu ausimamie uchaguzi ufanyike kwa amani na nchi iendelee kuwa kisiwa cha amani.

“Ndugu zangu tarehe 28 mwezi huu, Taifa letu la Tanzania linataingia katika uchaguzi mkuu wa Rais ,wabunge na Madiwani, Niwaombe,naomba tujitokeze kwa wingi ili tukachagua viongozi wapenda maendeleo watakaoliongoza Taifa hili katika kipindi kingine cha miaka mitano’’,alisema Mndeme.

Mndeme amewasisitiza Watanzania ifikapo Oktoba 28 kila mmoja achukue maamuzi sahihi kuchagua viongozi sahihi na wanaopenda maendeleo na nchi ya Tanzania iendelee kuimarika katika Nyanja zote.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Ushirika wa Mama wa Kristo (UMAKI) katika Kanisa la Anglikana Agnes Hinjo, amemshukuru Mkuu wa Mkoa kwa kuja kuabudu katika ibada hiyo na kumuahidi kwamba wataendelea na maombi ya kuliombea Taifa la Tanzania siku zote.

“Sisi waumini wa Kanisa la Anglikana tupo kwenye maombi,UMAKI tumeamua kuchukua hatua za kuendelea na maombi tangu aliposema Rais Magufuli tufunge kwa ajili ya corona,hatujaacha,tupo kwenye maombi kwa ajili ya uchaguzi’’,alisema Hinjo.

Naye Mchungaji wa Kiongozi wa Kanisa hilo Padre Mathayo Chanangula katika mahubilri yake kwenye ibada hiyo amempongeza Mkuu wa Mkoa kwa kazi njema anayofanya ya kusimamia masuala ya kimwili na kiroho

Padre Chanangula amesema msaada wa saruji ambao ameutoa kwa ajili ya ujenzi wa nyumba ya mchungaji utasaidia sana katika ukamilishaji wa nyumba hiyo ambayo itamwezesha Mchungaji kufanya kazi za kiroho kwa ufanisi zaidi.

Imeandaliwa na Aneth Ndonde

Kutoka ofisi ya Habari ya Mkoa wa Ruvuma

Oktoba 18,2020.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...