


***********************************
NA VICTOR MASANGU, MKURANGA
Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo amepiga amekemea na kupiga marufuku kwa baadhi ya wakulima kuuza zao la korosho kwa kutumia mfumo ambao haukubaliki unaojulikana kama kang’omba na badala yake wahakikishe wanazingatia mwongozo uliwekwa na serikali wa kuuza korosho hizo kwa kutumia mfumo wa stakabadhi ghalani ili kuepukana na changamoto za kuwanyonya na kuwadhulumu haki zao wakulima.
Ndikilo ametoa agizo hilo wakati wa mkutano na wadau mbali mbali wa zao la korosho pamoja na viongozi wa vyama vya msingi vya ushirika pamoja na wakuu wa idara mbali mbali kwa ajili ya kuweza kujadili namna ya kuweka mikakati ambayo itaweza kuwasaidia wakulima kuuza korosho zao katika msimu unaokuja ikiwemo kuzitatua changamoto zinazowakabili.
“Sisis kama serikali ya Mkoa wa Pwani lengo letu kubwa ni kuhakikisha kwamba tunawasaidia wakulima wetu wa zao la korosho kwa kuweka mipango mizuri na mikakati ambayo itaweza kusaidia kabisa kuondokanana nah ii hali ya kuwanyonya wakulima kwa kutumia mfumo wa kangomba hii haikubaliki hata kidogo kikubwa hapa inabidi vyama vya msingi viweze kulisimamia ili kwa kutumia mfumo halali wa stakabadhi ghalani”alisema Ndkilo.
Pia Ndikilo alisema kwamba katika kutimiza malengo amabyo wamejiwekea ni lazima wakulima wote wa zao la kurosho kuhakikisha kwamba wanazingatia taratibu zote za kilimo kwa kufanya usafi wa mashamba yao na kutoka uchafu wote ili korosho zisiweze kuharibika na hatimaye kuweza kupata korosho nzuri yenye ubora ambao unaweza kuwafanya wapate wanunuzi wengi.
Kadhalika aliongeza kuwa kilimo cha zao la korosho ni mkombozi mkubwa kwa wananchi kutokana na asilimia zaidi ya 80 wanategemea zao hilo katika kujiingizia kipato chao na kuondokana na wimbi la umasikini hivyo ndio maana serikali imeamua kulitilia mkazo suala hilo ili kuonyesha kwamba linaweza kuleta mabadiliko chanya ya kimaendeleo na kukuza uchumi wan chi.
Katika hatua nyingine Mkuu huyo wa Mkoa waliwaasa viongozi wa vyama vya msingi vya ushiriki kuwepo mipango madhubuti ya kuwatengenezea mazingira ambayo ni sahii wakulima wa zao la korosho katika kuelekea msimu mpya wa uuzaji ili waondokana na changamoto ya upatikanaji wa kupata soko kwa urahisi sambamba na kuzihifadhi katika maghala ambayo yametengwa maalumu.
Nao baadhi ya wakulima wa zao la korosho ambao wamehudhulia katika mkutano huo wa wadau hawakusita kutoa kilio chao kwa Mkuu wa Mkoa kuhusiana na changamoto inayowakabili ya ukosefu wa vifaa maalumu kwa ajili ya kupimia ubora wa zao hilo pamoja na kuimba serikali iweze kuwasaidia kwa hali na mali upatikanaji wa pembejeo za kilimo pamoja na magunia.
Naye Katibu Tawala wa Mkoa wa Pwani Dk. Dolpine Magere amebainisha kwamba katika msimu ulipita kulikuwepo n achangamoto mbali mbali ambazo ziliweza kujitokeza ikiwemo kuwepo kwa mvua kubwa ambazo zilipelekea baadhi ya korosho kuharibika hivyo kwa sasa wamejipanga katika kujiandaa na msimu mwingine ambao unakuja.
Alisema zao la kurosho katika mkoa wa Pwani linachangia kwa kiasi kikubwa kuongeza pato na kukuza uchumi kwa wananchi hivyo ni vema litakitiliwa mkazo mkubwa ili wakulima waweze kunufaika kupitia zao hilo ambapo aliwahimiza waweze kuzingatia taratibu zote wanazopatiwa na wataalamu ili korosho zao ziweze kuwa na ubora mzuri.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Mafia Shaibu Mnunduma amesema kwamba ili kuweza kukabiliana na changamoto mbali mbali zinazowakabili wakulima ni lazima kuwashirikisha mabwama shamba katika kila hatua mbao wataweza kutoe elimu zaidi juu ya upandaji, ulimani pamoja na utunzaji wa zao hilo kwa kuzingatia misingi ya taratibu zote zilizowekwa lengo ikiwa kupata ubora unaotakiwa.
Kilimo cha zao la korosho katika Mkoa wa Pwani kimekuwa ni moja ya mkombozi mkubwa katika kuwakomboa wananchi kuweza kuondokana na wimbi la umasikini na kuongeza pato la Taifa hivyo kunahitajika juhudi za makusudi kutoka serikalini ili kuweza kuondokana na changamoto mbali mbali zinazowakabili wakulima hao.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...