Naibu Kamishna Mkuu wa Mamlaka
ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Msafiri Mbibo (wa tatu kushoto) akiwa
katika picha ya pamoja na uongozi wa TRA Mkoa wa Dodoma na watumishi wa
Kituo cha Huduma za Kodi cha Kibaigwa wakati alipotembelea kituo hicho
kwa lengo la kuwapa hamasa watumishi hao kuendelea kufanya kazi kwa
bidii na weledi katika ukusanyaji mapato ya Serikali.
Msimamizi wa Kituo cha Huduma za Kodi cha Kibaigwa kilichopo chini ya
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bi. Elisamaria Emmanuel akitoa taarifa
ya utendaji kazi wa kituo hicho kwa Naibu Kamishna Mkuu wa Mamlaka hiyo
Bw. Msafiri Mbibo wakati alipotembelea kituo hicho kwa lengo la kuwapa
hamasa watumishi kuendelea kufanya kazi kwa bidii katika ukusanyaji
mapato ya Serikali.
Msimamizi wa Kituo cha Huduma za Kodi cha Kibaigwa kilichopo chini ya
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bi. Elisamaria Emmanuel akitoa taarifa
ya utendaji kazi wa kituo hicho kwa Naibu Kamishna Mkuu wa Mamlaka hiyo
Bw. Msafiri Mbibo wakati Naibu Kamishna Mkuu huyo alipotembelea kituo
hicho kwa lengo la kuwapa hamasa watumishi kuendelea kufanya kazi kwa
bidii katika ukusanyaji mapato ya Serikali.
Afisa
Msimamizi wa Kodi wa Kituo cha Huduma za Kodi cha Kibaigwa kilichopo
chini ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Mohammedy Madebe
akichangia hoja wakati Naibu Kamishna Mkuu wa Mamlaka hiyo Bw. Msafiri
Mbibo alipotembelea kituo hicho kwa lengo la kuwapa hamasa watumishi
kuendelea kufanya kazi kwa bidii na weledi katika ukusanyaji mapato ya
Serikali.
Naibu
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Msafiri Mbibo
akisaini kitabu wa wageni kwenye ofisi ya Katibu Tawala wa Wilaya ya
Mpwapwa wakati alipomtembelea Katibu Tawala huyo ofisini kwake.
Naibu Kamishna Mkuu wa Mamlaka
ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Msafiri Mbibo akizungumza na Katibu Tawala
wa Wilaya ya Mpwapwa Bi. Sarah Komba wakati Naibu Kamishna Mkuu huyo
alipomtembelea ofisini kwake ambapo alimshukuru kwa ushirikiano
unaotolewa na uongozi mzima wa wilaya hiyo kwa Mamlaka ya Mapato
Tanzania.
Katibu Tawala wa Wilaya ya
Mpwapwa Bi. Sarah Komba akizungumza na Naibu Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya
Mapato Tanzania (TRA) wakati Naibu Kamishna Mkuu huyo alipomtembelea
ofisini kwake.
Kaimu Meneja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Wilaya ya Mpwapwa Bw.
Nelson Makweta akiwatambulisha watumishi wa TRA wilayani humo wakati
Naibu Kamishna Mkuu wa Mamlaka hiyo Bw. Msafiri Mbibo alipowatembelea
kwa lengo la kuwapa hamasa watumishi hao kuendelea kufanya kazi kwa
bidii na weledi katika ukusanyaji mapato ya Serikali.
Afisa
Msimamizi wa Kodi wa Ofisi ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Wilaya
ya Mpwawa mkoani Dododma Bw. Hezekia Shekyandumi akichangia hoja wakati
Naibu Kamishna Mkuu wa Mamlaka hiyo Bw. Msafiri Mbibo alipotembelea
ofisi hiyo kwa lengo la kuwapa hamasa watumishi kuendelea kufanya kazi
kwa bidii na weledi katika ukusanyaji mapato ya Serikali. (PICHA ZOTE NA
VERONICA KAZIMOTO)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...