Na Woinde Shizza , Michuzi Tv Arusha
Prof
Tumbo aliyasema hayo leo jijini hapa alipokuwa akifunga maadhimisho ya
siku ya kimataifa ya vyama vya ushirika wa akiba na mikopo duniani
ambapo alisema ni vyema viongozi wa ushirika wakakaa na kuangalia namna
watakavyoondoa migogoro hiyo ili vyama hivyo viendelee kukuwa.
Kwa
upande wa Meneja Biashara wa Benki ya CRDB,Kanda ya Kaskazini,David
Peter alisema kuwa Benki yao imekuwa ikishirikiana Sana na vyama vya
ushirika wa akiba na mikopo na hadi sasa wamesha shirikiana na vyama vya
ushirika zaidi ya 450 ,pia wameshatoa mikopo ya zaidi ya bilioni 300
kwa vyama hivyo.
Aidha
alisema kuwa wamekuwa wakichangia kusaidia vyama hivi , wamekuwa
wanashiriki kuwajengea uwezo wa vyama kuanzia kwa watendaji na bodi zake
,katika vipindi tofauti tofauti wamekuwa wakitoa mafunzo nchi nzima kwa
vyama vyote vya ushirika ambavyo vimeingia ubia na Benki ya CRDB
,Kuhakikisha wanakuwa na uwezo sahihi na uelewa katika kusimamia
shughuli za kifedha Ndani ya vyama vyao vya Sacco's.
"Hii
imewezesha vyama kuwa endelevu na pia imewezesha kutunza fedha zao
vizuri na pia kutoa mikopo na kuwezesha wananchi wale ambao wanapewa
mikopo wanarejesha kwa wakati na tunaendelea kuona vyama hivi
vinaendelea kukuwa "alisema David
Aliwaasa
wananchi wasiweke pesa Ndani ambapo apana usalama Bali wapeleke pesa
Benki ,pia waweke Ela sehemu ambayo wanapata faida nawaache kuweka fedha
sehemu ambazo awapati faida .
Kwa
upande wa migogoro alisema kuwa Ni vyema vyama wakakaa na kuangalia
namna ya kutatua migogoro waliyonayo , waangalie ni sehemu gani
wanakosea wakajirekebisha,pia Ni vyema wakatafuta Benki Kama CRDB
ikawajengea viongozi uwezo wa kutambua Mambo mbalimbali Kama kujua namna
soko la fedha linavyoenda Baadhi
ya wataalam wa maswala ya fedha wamesema tatizo kubwa linalovikabili
vyama vingi vya ushirika wa akiba na mikopo Ni pamoja na kufanya
biashara kwa mazoea na kutafuta njia za mkato.
Mtaalam
wa maswala ya fedha Prof Alfred Sife alisema tatizo la kutofuata
Sheria Ni kubwa pia Asilimia kubwa ambapo hivi karibuni vyama zaidi ya
elfu Tatu (3000)vimefutwa
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...