SHULE
ya Sekondari St. Methew's mbioni kianzisha masomo ya upishi na ushonaji
ikiwa na lengo la wanafunzi wanaohitimu masomo katika shule hiyo kuacha
kuzurula kutafuta kazi au kipato.
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi
Mtendaji wa Mutembei Holding Limited (MHL), Peter Mutembei wakati
akizungumza katika Mahafali ya 20 ya shule ya Sekondri St. Methew's
iliyopo Mpakani mwa jiji la Dar es Salaam na mkoa wa Pwani, mahafali
iliyofanyika mwishoni mwa wiki Oktoba 3, 2020. Alisema kuwa masomo hayo
yanawasaidia katika shughuli za uzalishaji mali na ni njia bora ya
kumuepusha na vishawishi kutoka makundi mabaya katika jamii.
Hata hivyo Mutembei alisema kuwa shule ya Sekondari St. Methew's
imejikita zaidi katika malezi bora ya Mtoto ambayo yatamwezesha kujua
hili ni baya na hili ni zuri la kufanya.
"Shuleni hapa
tunawafunzisha uzalendo, maadili mema na nidhamu, ikiwa tunaushirikiano
mwema na serikali ambapo wataalamu mbalimbali wameanza kufika shuleni
kwetu kutoa mafunzo ya nidhamu."
Amesema katika kusimamia malezi,
hawataki kuwajengea watoto nidhamu ya woga wakiwa na dhamira ya
kumuandaa mtoto kujua hili ni baya hawezi kufanya hata kama hakuna mtu
anamwona.
Kwa Upande Afisa elimu Mkoa wa Mkuranga, Hadija mcheka
alisema kuwa wao kama Serikali wataendelea kudumisha ushirikiano
uliopo na shule ya Sekondari St. Methew's ili kuleta matokeo chanya
zaidi katika utoaji wa elimu.
"Tutahakikisha kwamba watoto wa
Kitanzania wanapata elimu iliyobora katika mazingira bora, kama serikali
tunaendelea kuboresha huduma ya elimu, tumeanza kufanya Ukarabati
katika shule zetu, tunaendela kuajiri walimu pale ambapo kunakuaa na
upungufu wa walimu...." Alisema Hadija
Hata hivyo Hadija Alisema
kuwa lengo la Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni
kuhakikisha kila mtoto anapata hakia ya elimu bila kuwa na kipingamizi
chochote.
"Serikali imehakikisha kila mtoto anapata elimu, kwa
yule anayeshindwa kwenda shule za Serikali ama mzazi amebarikiwa kipata
basi Mlete mwanao kwa shule za Mutembei na huu ndio ushirikiano tulionao
kati ya shule binafsi na Serikali...." Alisema Hadija






Mwanafunzi wa shule shule ya Sekondari St. Methew's wakitoa burudani katika mahafali ya 20.



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...