Charles James, Michuzi TV


Mgombea Ubunge wa Viti Maalum Wanawake Mkoa wa Dodoma CCM, Mariam Ditopile amefanya mkutano wa kuomba kura za Mgombea Urais wa CCM, Dk John Magufuli katika Kata ya Hogoro wilayani Kongwa ambapo amelaani vitendo vya kujeruhiwa na kuuawa kwa viongozi na wanachama wa chama hicho kinachofanywa na vyama pinzani.


" Hadi sasa vijana wetu wa nne wameshauawa na vyama vya upinzani, tumeshuhudia Iringa, Tunduma na hapa Chemba Dodoma. Tuwapongeze Jeshi la Polisi kwa kuchukua hatua lakini tunaungana na Katibu Mkuu wetu, Dk Bashiru Ally kukemea vitendo hivi na kuwasihi watanzania kuwaepuka watu wenye lengo la kutugawa na kuumiza maisha ya watanzania wenzetu,


Watu hawa ni wa hovyo, wanaomba kuongoza Nchi lakini wametawaliwa na chuki, Mgombea wao wa Urais kule Zanzibar anahubiri Udini na kuhamasisha vitendi vya kuumiza watu, ivi karibuni wamevamia watu wetu Msikitini na kuwaumiza,  tusiwachague watu wa namna hii watatugawa.


Tuwapongeze Jeshi la Polisi kwa kuchukua hatua lakini tunaungana na Katibu Mkuu wetu, Dk Bashiru Ally kukemea vitendo hivi na kuwasihi watanzania kuwaepuka watu wenye lengo la kutugawa na kuumiza maisha ya watanzania wenzetu," Amesema Ditopile.


Amewaomba watanzania na hasa viongozi wa Dini kukemeea mauaji hayo na vitendo hivyo na kuwaomba watanzania kujitokeza kwa wingi Oktoba 28 kumpigia kura Dk Magufuli ili aweze kuibuka na ushindi wa kishindo na kuwatumikia watanzania kwa miaka mingine mitano.


" Wote mmeshuhudiwa kule Iringa viongozi wa Chadema wamekamatwa kwa kuhusishwa na mauaji ya wana CCM wenzetu, kwa vitendo wanavyovifanya wanaonesha jinsi gani hawafai kupewa madaraka kwani watavunja amani ya Nchi iliyoasisiwa na Baba wa Taifa, Mwl Julius Nyerere.

 Mgombea Ubunge Viti Maalum Wanawake Mkoa wa Dodoma CCM, Mariam Ditopile akiomba kura za Mgombea Urais wa CCM, Dk John Magufuli kwa wananchi wa Kijiji cha Makutani kata ya Hogoro wilayani Kongwa.

 Mgombea Ubunge Viti Maalum Wanawake Mkoa wa Dodoma CCM, Mariam Ditopile akimkabidhi Diwani mteule wa Kata ya Hogoro, Mtwanga Sadala ilani ya Chama cha Mapinduzi CCM ili aitumikie pindi atakapoapishwa kuwa Diwani wa kata hiyo. Diwani huyo amepita bila kupingwa.

 Mgombea Ubunge Viti Maalum Wanawake Mkoa wa Dodoma CCM, Mariam Ditopile akiagana na mmoja wa wananchi waliohudhuria mkutano wake wa kutafuta kura za Mgombea Urais wa CCM, Dk John Magufuli.

Mgombea Ubunge Viti Maalum Wanawake Mkoa wa Dodoma CCM, Mariam Ditopile akizungumza na wananchi wa Kata ya Hogoro wilayani Kongwa alipoenda kuomba kura za Mgombea Urais wa CCM, Dk John Magufuli.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...