Katibu wa CCM Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, Ally Kidunda akimnadi Mgombea udiwani wa Kata ya Ngorika Albert Msole.
…………………………………………………………………………
Na Mwandishi wetu, Simanjiro
WAGOMBEA udiwani wa
Kata nane kwenye Jimbo la Simanjiro Mkoani Manyara, kupitia CCM,
wamepita bila kupingwa kati ya Kata 18 za eneo hilo, hivyo kuwa na
uhakika wa ushindi kwani ni Kata 10 pekee zilizobakia ambazo zina
upinzani kwenye uchaguzi mkuu.
Katibu wa CCM
Wilayani Simanjiro, Ally Mohamed Kidunda ameyasema hayo kwa Makamu
Mwenyekiti wa UVCCM Taifa Tabia Mwita kwenye mkutano wa kampeni ya kata
za Msitu wa Tembo na Ngorika.
Kidunda alizitaja kata hizo nane ambazo madiwani wa CCM wamepitwa bila kupingwa ni Mirerani, Naisinyai, Shambarai na Terrat.
Amezitaja kata
nyingine ambazo madiwani wake kupitia chama hicho wanasubiri kuapishwa
baada ya kufanyika uchaguzi ni Loiborsiret, Komolo, Oljoro namba tano na
Emboreet.
Amesema chama hicho
kina uhakika wa kushinda kwani hadi hivi sasa wana mtaji huo wa madiwani
nane kibindoni wanatafuta kura za madiwani 10 waliobakia na kupingwa na
wapinzani.
“Kwa hapa Ngorika
tuna uhakika wa ushindi kwani mgombea wetu Albert Msole ni diwani makini
ameweza kuwa Makamu Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Simanjiro
kwa miaka minne mfululizo,” amesema Kidunda.
Makamu Mwenyekiti wa
UVCCM Taifa, Tabia Mwita amewaomba wananchi wa eneo hilo kuwapigia kura
wagombea was CCM wa udiwani, mgombea ubunge Christopher Ole Sendeka na
urais Dk John Magufuli.
“Tunapaswa kutambua
kazi kubwa aliyofanya Rais Magufuli kwenye kipindi cha miaka mitano ya
kwanza hivyo tumpe nafasi nyingine ya miaka mitano amalizie miradi mingi
aliyoianzisha,” amesema Mwita.
Mgombea udiwani kata
ya Ngorika Albert Msole amesema kwa kipindi cha miaka mitano ya
2015/2020 amefanikisha miradi mingi ya maendeleo katika sekta mbalimbali
hivyo anaomba miaka mitano tena.
Mgombea udiwani kata
ya Msitu wa Tembo Kaleiya Mollel amewaomba wananchi wa eneo hilo kutoa
kura kwa CCM kwani Tabia ametoka Zanzibar ili aombe kura kwao
wasimuangushe.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...