Charles James, Michuzi TV

Mgombea Ubunge Viti Maalum Wanawake Mkoa wa Dodoma CCM, Mariam Ditopile amesema ndani ya kipindi cha miaka mitano cha Rais Dk John Magufuli zaidi ya Sh Trilioni 1.1 zimetumika kwa ajili ya elimu bila malipo Ikiwa ni sera ya Dk Magufuli kuhakikisha kila mtanzania anapata elimu bila kulipa ada kuanzia Shule ya Msingi hadi Kidato cha Nne.

Hayo ameyasema leo katika Kata ya Majereko wilayani Chamwino alipokua amealikwa katika mahafali ya kidato cha nne Shule ya Sekondari Majereko ambapo pamoja na mambo mengine ameahidi kuwapelekea Kompyuta, Mashine ya kuchapa na ile ya kutolea kopi.

Ditopile amesema Wilaya ya Chamwino ni moja kati ya Wilaya ambazo ndani ya muda mfupi zitanufaika na maendeleo kutokana na kuwa karibu na Ikulu lakini pia endapo mgombea Ubunge wa Jimbo la Chamwino kupitia CCM, Deo Ndejembi akishinda ataongeza kasi hiyo zaidi.

" Suala la elimu bure ni moja kati ya ahadi za Dk Magufuli kwetu alipokua anaomba ridhaa kwa mara ya kwanza na hakika amefanikiwa sana, watu wengi wanadhani ni elimu bure la hasha ni elimu bila wazazi kulipa ada kwa sababu Rais Magufuli alisema ada italipwa na serikali yake, zipo Nchi kubwa zenye rasilimali kushinda sisi lakini wanashangaa sisi tumewezaje, niwaombe muungeni mkono Rais Magufuli na serikali yake katika hili wametushika mkono wengi sana.

Sekta ya elimu imepiga kasi sana, Shule za Sekondari zimeongezeka kutoka 4708 mwaka 2015 hadi 5330 mwaka huu, shule kongwe zimeboreshwa na leo tunaona matokeo ya mwisho ya kidato cha sita shule za serikali saba zimeingia 10 bora, lakini madawati yameongezeka kutoka Milioni 3 hadi Milioni 8.9 huku vyuo zaidi ya 70 vya ufundi vikijengwa Nchi nzima na sisi Dodoma tumepata pia," Amesema Ditopile.

Aidha amewapongeza wanafunzi hao 46 wanaohitimu masomo yao huku akiwataka kufanya vizuri kwenye mitihani yao inayokuja ili iwe zawadi kwa Rais Magufuli ambaye serikali anayoiongoza yeye imekua ikiwalipia ada kwa miaka minne yote wakiwa shule.

" Niwaombeni mtulie ili muweze kufanya mitihani yenu vizuri, kwa miaka minne walimu wamefanya kazi kubwa ya kuwafundisha sasa ni zamu yenu kwenda kutimiza sehemu ya ndoto zenu kwa kufaulu vizuri, amini kwamba unaweza kufaulu na kuendelea na masomo yenu, mtangulizeni Mungu kwani yeye huweka wepesi hata pale kwenye ugumu," Amesema Ditopile.

Mgombea Ubunge Viti Maalum Wanawake Mkoa wa Dodoma CCM, Mariam Ditopile akimkabidhi tuzo mwanafunzi mwenye nidhamu zaidi katika mahafali ya kidato cha nne Sekondari ya Majereko wilayani Chamwino leo.

Mgeni rasmi kwenye mahafali ya kidato cha nne Shule ya Sekondari Majereko wilayani Chamwino, Mariam Ditopile akikata keki sambamba na wanafunzi wanaomaliza huku Mwenyekiti wa Bodi ya shule hiyo akishuhudia.

Mgeni rasmi kwenye mahafali ya kidato cha nne Shule ya Sekondari Majereko, Mariam Ditopile akiwapa nasaha wanafunzi wanaomaliza ili waweze kufanya vizuri kwenye mitihani yao ya mwisho Novemba mwaka huu.
Wazazi, Wananchi na Wageni waliohudhuria mahafali ya kidato cha nne Shule ya Sekondari Majereko iliyopo wilayani Chamwino mkoani Dodoma.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...