Mwandishi Wetu, Michuzi TV

KATIKA kuendeleza kilimo endelevu nchini, Ubalozi wa Ufaransa nchini Tanzania kwa kushirikiana na ubalozi wa Ubelgiji pamoja na Shirika la Chakula Duniani (FAO) wameandaa mikutano ya wadau wa kilimo endelevu na wanafunzi wa vyuo katika mikoa ya Morogoro na Arusha.

Hivyo Ubalozi huo wa Ufaransa nchini ameamua  umemleta nchini mtaalamu wa kimataifa katika masuala ya kilimo endelevu Profesa Marc Dufumier ambaye anatoka Chuo cha AgroParis Tech cha nchini Ufaransa.

Profesa  Dufumier akiwa nchini Tanzania atakutana na wadau wa kilimo endelevu pamoja na wanafunzi wa Chuo cha Kilimo cha Sokoine (SUA) pamoja na wale wa Chuo cha Nelson Mandela cha Arusha.

Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania Federic Clavier, amewaambia waandishi wa habari leo Oktoba 9,2020 jijini Dar es Salaam kwamba Prof. Dufumier atakutana na wadau wa masuala ya kilimo endelevu kutoka kwenye asasi zisizo za kiserikali na zisizo za kiserikali.Pia atakutana na wanafunzi wa vyuo hivyo ambapo pamoja na mambo mengine wataangalia changamoto zilizopo katika kilimo endelevu nchini.

Balozi Clavier amefafanua juhudi hizo  zinazofanywa na nchi ya Ufaransa zinalenga kuendeleza kilimo endelevu kama ambavyo wenzeo wa FAO na Ubelgiji wamekuwa nao, hivyo wanaamini  kilimo hicho ni sahihi ya kuzalisha chakula kwa wingi na utunzaji wake.

"Mikutano hiyo itafanyika Oktoba 13 mwaka huu mkoani Arusha na itakuwa mikutano miwili kwa siku chuoni Nelson Mandela ambapo mkutano mwingine utafanyika Morogoro Oktoba 16 katika Chuo cha Sokoine"amesema.

Kwa upande wake Balozi wa Ubelgiji nchini Tanzania Peter Van Acker ametumia nafasi hiyo kueleza kuwa kuna umuhimu mkubwa kwa Tanzania kuendeleza kilimo endelevu kwa kuwa ni njia pekee ya kutunza ardhi kwa ajili ya kizazi cha sasa na kizazi kijacho.

Wakati huo huo Mkurugenzi wa FAO hapa nchini Stephen Kargbo amesema ni vizuri kwa nchi za Bara la Afrika ikiwemo Tanzania kuhakikisha zinaweka mkazo katika eneo la kilimo endelevu.

"FAO imejikita katika kusaidia kilimo endelevu na kwa kushirkiana na wadau wengine tumekuwa tukisaidia programu mbalimbali za kilimo endelevu kwa maendeleo ya Tanzania, Afrika na Dunia kwa ujumla"amefafanua Mkurugenzi huyo.

 Balozi wa Ubelgiji nchini Tanzania, Peter Van Acker akizungumza na waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam baada ya mkutano na wadau wa kilimo waliokuwa wakijadili kuhusu kilimo endelevu. 

 Balozi wa ufaransa nchini Tanzania, Frédéric Clavier akizungumza na waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam baada ya mkutano wa ndani na wadau wa kilimo waliokuwa wakijadili kuhusu kilimo endelevu.

Mkurugenzi Mkaazi nchini Tanzania wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo Dunia (FAO) Stephane Kargbo akizungumza na waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam baada ya mkutano wa ndani na wadau wa kilimo waliokuwa wakijadili kuhusu kilimo endelevu.
Mtaalam wa Kilimo kutoka Ufaransa, Profesa Marck Dufumier akizungumza na waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam baada ya mkutano wa ndani na wadau wa kilimo waliokuwa wakijadili kuhusu kilimo endelevu.

 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...