*Atoa ya moyoni mbele ya maelfu ya wananchi waliokuwa wakimsikiliza

*Azungumzia mafanikio yaliyopatikana, wabunge wanaotoka Bungeni

Na Said Mwishehe, Michuzi TV -Kilimanjaro

MGOMBEA Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi(CCM) Dk.John Magufuli amewahutubia maelfu ya wananchi wa Mkoa wa Kilimanjaro wakiwemo wa Manispaa ya Moshi Mjini ambapo ametumia nafasi hiyo kuelezea mafanikio makubwa yaliyopatikana miaka mitano iliyopita huku akitumia nafasi hiyo kuzungumzia sekta ya nishati ya umeme ilivyoimarishwa.

Akizungumza leo Oktoba 21,mwaka 2020 na wananchi hao Dk.Magufuli amesema eneo jingine ambalo wamefanya vizuri katika kipindi cha miaka mitano ni ni sauala la umeme, kwani wametekeleza miradi mikubwa ukiwemo wa Kinyerezi I na Kinyerezi II na ndio maana mgao wa umeme umepungua nchini kwani zamani ilikuwa mahenereta yanashindana kwa kunguruma lakini sasa yamepungua.

"Tumefanikiwa kudhibiti hata ufisadi uliomo ndani ya mashirika yetu, kwa mfano tulikuwa tunalipa Sh.bilioni 719 kila mwaka kwa ajili ya kulipia majenereta ya IPTL Symbion na Agreco, pia tumepunhguza gharama za kuweka umeme kutoka Sh.177,000 hadi Sh.27000 na ndio maana tumefanikiwa kupeleka umeme.

"Tumeanzisha bwala la Julius Nyerere, na mradi huo ukikamilika bei ya umeme itashushwa, na lengo la kushusha tunataka tuwe na viwanda vingi , tunataka viwanda vilivyolala tuvifufue vyote. Hapa Moshi kulikuwa na kiwanda cha Ngozi Karanga ambacho kilikuwa chini ya Magereza, hivi sasa tumekiboresha ukifika katika kiwanda hicho ni kama uko Ulaya, kitakuwa kikitengeneza viatu, mikoba na mikanda ya ngozi, tunataka kufufua hivyo viwanda , tunataka kuirudisha Moshi kuwa kama ya zamani.

"Tutakapokuwa na viwanda vingi vijana watapa ajira, bila viwanda hutapata ajira, ndio maana tunataka tuwe na viwanda hapa na malighafi itakayozalishwa hapa itumike kutengeneza bidhaa za hapa, tunataka kutengeneza Moshi mpya, Kilimanjaro mpya, Tanzania mpya, hakuna sababu ya kupeleka Kahawa Ulaya kabla ya kuitengeneza, hakuna sababu ya kusafirisha pamba Ulaya, wakipelekewa Ulaya wanatengeza nguo halafu wanazivaa

"Tunataka nguo zitengenezwe hapa na kisha Ulaya wapelekewe mitumba wakavae.Nimekuja hapa nikatimize ndoto ya kuwa mtumishi wenu katika kipindi cha miaka 10 badala ya kunikatisha hiyo ndoto kwa miaka mitano tu.

Ametumia nafasi hiyo kuwathibitisha wananchi wa Mkoa wa Kilimanjaro kwamba changamoto zote ambazo ameelezwa amezisikia zikiwemo za maombi ya barabara za lami, hivyo atashughulikia na hakuna ambacho kitashindikana."Tutatandika lami katika barabara nyingi tu za hapa hata ile barabara ya Kimoshi , Shime kwenda International school ya kilometa 43 tunatandika kwa lami, TPC, Mabwegini hadi Kahe ya kilomteta 114 nayo tutaiweka lami na nyingine nyingi.

"Ninachotaka kuwaambia wana Kilimanjaro na wana Moshi nimejipanga kuwafanyia kazi, mmteseka kwa muda mrefu , heshima ya Kilimanajro na Moshi lazima tuirudishe, mmechelewa sana.Unamchagua mbunge anakwenda Bungeni badala ya kuzungumzia barabara anaweka bandeji mdomoni, mbunge uliyemtuma kwa gharama yako ya kura anafunga mdogo

"Moshi hapa ni mashahidi ulitokea ugonjwa wa Corona Dunia  nzima watu wamekufa kwa maelfu, tukaambiwa Afrika watu watakufa kama mizogo, huo ulikuwa mtihani mkubwa katika uongozi wangu, watu waliambiwa wafungiwe ndani.Wewe ni rais na una watu milioni 60 uaambiwa watu wako uwafungie ndani, yalikuwa maisha ya ajabu, mategemeo yangu yakawa ni Bunge la Tanzania, wawe wamekaa kule wanipe ushauri niipeleke wapi Tanzania.

"Wakati unatafakari hayo kwenye TV unaona idadi ya watu wanakufa, katika nchi mbalimbali , jiweke katika maisha niliyokuwa nayo, wakati nasubiri naona wanatoka bungeni wanakimbia.Mnawajua waliokuwa wanakimbia ni wa chama gani? Wao kwao maisha yao ni mazuri zaidi kuliko watu waliowachagua, hata kupanga mpango maalum wameshindwa, ni watu wa binafsi, hawakujali maisha ya watu masikini, watoto, masikini ambao walisimama barabara kuwapigia kura,

"Nawaambia ndugu zangu waliobaki kule mnawajua walikuwa wa Chama gani, walivumilia maisha yote wakiongozwa na Spika Job Nugai, nikapata ushauri kutoka kwa viongozi wa dini, nikawoamba watanzania tumlilie Mungu, tulimlilia Mungu kwa kufunga na kusali , Corona ikapotolea mbali,Mungu wetu akajibu,"amesema Dk.Magufuli.

Amefafanua alipoamua kuchukua mapapai kuyapima nayo yakawa na Corona, Mbuzi ana corona,hivyo akajua kabisa huo ni ugonjwa umeletwa na Ibilisi ni wa kupandikiza, hivyo kiboko ya Ibilisi ni Mungu, leo hapa hakuna kuogopana. "Namshukuru Mungu, nawashukuru wana Kilimanjaro na Watanzania wote, tusimtupe Mungu kwani analipenda Taifa hili, ndio maana wakati Corona inaendelea Tanzania imetoka kuwa nchi masikini na kuingia uchumi wa kati.

"Na Tanzania ni miongoni mwa nchi tano ambazo uchumi wake unakuwa kwa kasi, hivyo nawaambia tusimame pamoja, tusibaguane kwasababu ya dini, tusibaguane kwa sababu  ya makabila.Hata kwa Wachaga kuna makabila mengine ndani yake. Tunayo makabila mengi lakini tumebaki kuwa Taifa moja la Tanzania likiwa na amani.Tuna wabunge 28 wamepita bila kupingwa na wameshatangazwa katika gazeti la Serikli.

"Halafu wewe ambaye huna hata mbunge unasema utashinda, tunahitaji amani, ukiwa na amani nchi inakwenda mbele, tumeingia uchumi wa kati sisi tunakwenda mbele , tulikuwa na mikakati ya kwenda mbele na benki ya dunia walisema tutaingia uchumi wa kati miaka ya huko mbele kabisa lakini tumeingia sasa wanatushangaa tumefanya makubwa, tunapanga kutoa misaada kwa nchi nyingine ,

"Nataka Watanzania wawe mabilioneam nataka kujenga viwanda kwa ajili ya ajira wewe unataka kuandamana , nataka kuendelea kutoa elimu bure kwa watoto halafu wewe unataka kuandamana, nataka kuongeza fedha zaidi za mikopo ili vijana wengi wapate,"amesema Dk.Magufuli.

Ameongeza kuwa miaka mitano iliyopita wamefanya maboresho, wameshusha makato ya kodi kwa wafanyakazi, na kwamba wanataka kupandisha mishahara na marupurupu ya watumishi, halafu anatokea mtu anazungumza maandamano kuharibu nchi hii."Kwasababu ndugu zangu wa Kilomanjaro maisha sio kuwa Rais tu au Mbunge.Tunapogombana mabeberu wanafurahi na kuja kubeba dhahabu zetu."

"Sisi wote ni uzao wa Ibrahim, tunatakiwa kwenda pamoja kujenga taifa letu, tukichonganishwa na mabeberu wao wanakuja kubeba dhahabu, ndio mbinu wanazitumia.Mimi niko serikalini, lakini wapo wengine wamekuja kugombea wana tiketi za kurudi Ulaya, wana tiketi ya kwenda na kurudi,  wakichochea vurugu wao wanaondoka.

"Viongozi wa dini tunawaomba endeleeni kuliombea Taifa hili Mungu aliweke katika mikono yake, matokeo yameanza kuonekana wanagombana na nani mgombea urais na nani sio.Mungu wetu analipa mapema, na naomba waendelee kugombana hadi siku tunapiga kura,"amesema Dk.Magufuli mbele ya wananchi hao ambao mara kadhaa walisikika wakisema "Baba tusamehe, tumekukosea" ambapo aliwajibu kuwa yeye amewashasamehe tangu zamani.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...