Na Zainab Nyamka, Michuzi Tv

MWEZI wa Oktoba ukiwa ni maalumu kwa wiki ya huduma kwa wateja kimataifa, Chama cha Waajiri Tanzania (ATE) inatarajia kuwa na Kliniki  ya msaada wa Sheria za kazi na Ajira ambapo wanachama wetu na wasio wanachama watapata fursa ya kuuliza maswali mbalimbali.

Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa ATE Dkt Aggrey Mlimuka amesema wiki ya huduma kwa wateja imeanza rasmi leo Jumatatu tarehe 12 Oktoba 2020 mpaka tarehe 16 Oktoba 2020 na itakuwa ni wiki ya huduma kwa wanachama ili kuwapatia fursa ya kutoa  mrejesho kuhusiana na huduma zote zinazotolewa na ATE.


Amesema, katika wiki tunatarajia tutakuwa kuwa ma Kliniki ya msaada wa Sheria za kazi na Ajira ambapo wanachama wetu na wasio wanachama watapata fursa ya kuuliza maswali mbalimbali na wanasheria wetu watapawapatia majibu kulingana na mahitaji yao.

Dkt Mlimuka ameeleza, malengo makuu ya kufanya wiki hii ya huduma kwa wanachama ni Kutoa fursa kwa wanachama wetu kutupatia mrejesho kuhusiana na huduma zote zinazotolewa na ATE , Kupokea mapendekezo kutoka kwa wanachama wetu ya nini kifanyike au kipi kiboreshwe ili kufanya ATE kuendelea kuwa sauti ya Waajiri nchini mwetu.

Aidha, kutoa nafasi kwa wanachama wetu kufahamu kwa undani shughuli mbalimbali zinazofanywa na ATE kwa niaba yao, kusikiliza na kutoa ushauri kwa wanachama wetu

Dkt Mlimuka, kupitia vyombo  vya habari amewashukuru wanachama wote wa ATE waliopo nchi nzima kwa ushirikiano mkubwa ambao wamekuwa wakiwapatia katika kutekeleza mambo mbalimbali yaliyo kwenye kalenda ya Chama chao na amewaomba watumie wiki hii ya Huduma kwa Wanachama kuwasiliana nasi au kufika kwa wingi moja kwa moja kwenye ofisi zao.

ATE ni chombo pekee cha waajiri kinachowawakilisha nchini Tanzania chenye wanachama zaidi ya 1,500 wa moja kwa moja na zaidi ya 7,500 walio chini ya mwamvuli ya vyama mbalimbali ya kisekta ambapo 70% ya wanachama wapo Dar es Salaam huku 30% ni kutoka katika mikoa mengine ya Tanzania Bara.

Asilimia 90 ya wanachama wa ATE wanatoka katika Sekta binafsi huku 10%  wakitoka katika taasisi za Umma ATE ilianzishwa kwa lengo kuu la kuwakilisha na kutetea maslai ya waajiri nchini katika masuala ya kazi na Ajira.

Mkurugenzi Mtendaji wa ATE Dkt Aggrey Mlimuka akiwa kwenye picha ya pamoja ya wafanyakazi wa Chama cha Waajiri Tanzania (ATE)
Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Waajiri Tanzania (ATE) Dkt Aggrey Mlimuka akizindua wiki ya huduma kwa wanachama wa ATE kuanzia Oktoba 12-16 na kutoa fursa kwa wanachama wao kutoa mrejesho kuhusiana na huduma zote zinazotolewa na ATE.

 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...