baadhi ya wazee wanaoishi katika makazi ya wazee na
wasiojiweza Sukamnahela wakisubiri kupokea msaada wa vitu mbali mbali
vilivyotolewa na Wizara ya Afya.

Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dkt Rehema Nchimbi akipitia
risala ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya,Dkt John Jingu iliyosomwa kwa
niaba yakena Kamishina wa Ustawi wa Jamii,Dkt.Naftali Ng’ondi wakati
wa kukabidhi msaada wa vitu mbali mbali.


Baadhi ya viongozi wa serikali waliohudhuria hafla ya
makabidhiano ya vifaa mbali mbali kwa wazee waishio kwenye kambi ya
wazee na wasiojiweza ya Sukamahela.

 Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dkt. Rehema Nchimbi (aliyevaa
miwani) akimkabidhi mwenyekiti wa wazee wanaoishi kwenye kambi ya
wazee na wasiojiweza Sukamahela vifaa mbali mbali ili viweze
kuwasaidia katika mahitaji yao mbali mbali.(Picha zote Na Jumbe
Ismailly)


Na Jumbe Ismailly, Manyoni

KATIBU Mkuu Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na
watoto, Dkt John Jingu amesema wazee 281 wanaoishsi katika makazi 13 ya
wazee nchini wakiwemo wanaume 161 na wanawake 120 wamekuwa wakipatiwa kikamilifu matunzo katika kipindi cha kuanzia mwezi Januari,hadi kufikia mwezi septemba,mwaka huu.

Akitoa maelezo mafupi kwa niaba ya katibu mkuu wa wizara wakati wa
kukabidhi msaada wa vifaa mbali mbali kwenye makazi ya wazee na
wasiojiweza Sukamahela, Kamishina wa Ustawi wa Jamii, Dkt.Naftali
Ng’ondi amesema kwamba kwa mujibu wa sera ya Taifa ya Wazee ya mwaka
2003,inatambua wazi kwamba wazee ni rasilimali muhimu kwa maendeleo ya
Taifa.

Hata hivyo Dkt Jingu amebainisha kuwa makazi ya wazee ya Sukamahela
kuna jumla ya wazee 15 wakiwemo wanaume 12 na wanawake 3 na kwamba
kupitia wizara ya Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia,Wazee na watoto
inajivunia kupata mafanikio katika maeneo mbali mbali ya utoaji wa
huduma kwa wazee.

“Kwa mujibu wa sera ya Taifa ya mwaka 2003 inatambua kuwa wazee ni
raslimali muhimu kwa maendeleo ya taifa,hivyo ili kulinda haki na
ustawi wa wazee,sera hiyo inatoa jukumu kwa familia na jamii kuchukua
jukumu la kutoa matunzo kwa wazee” amesema.

Aidha Dkt Jingu amebainisha kwamba kwa wazee ambao wamekosa ndugu na
jamaa wa kuwatunza,serikali imekuwa ikichukua jukumu la kuwataunza
wazee hao katika makazi mbali mbali nchini.

Kwa mujibu wa Daktari huyo serikali imeendelea kuboresha miundombinu
na majengo ya makazi ya wazee kwa kufanya ukarabati na ujenzi mpya na
kwamba miongoni mwa makazi yaliyoboreshwa ni pamoja na makazi ya
Sukamahela.

Hata hivyo amesisitiza kwamba makazi ya wazee na wasiojiweza
Sukamahela yalianzishwa mwaka 1974 na lengo kuu la kuanzishwa kwake ni
kutoa huduma za matibabu pamoja na huduma zingine za msingi kwa
waathirika wa ugonjwa wa Ukoma na familia zao.

“Vile vile wizara imeendelea kuimarisha upatikanaji wa chakula katika
Makazi ambapo wizara imekuwa ikituma fedha kwa wakati ambazo
zinawezesha wazee kupata uhakika wa chakula ikilinganishwa na siku za
nyuma”.alifafanua katibu mkuu huyo.

Akikabidhi msaada wa vitu mbali mbali kwenye makazi ya wazee na
wasiojiweza,Mkuu wa Mkoa wa Singida,Dkt Rehema Nchimbi
amewahakikishiwa wazee hao kwamba serikali inawapenda sana na ndiyo
maana ofisi itakayoendelea kuwahudumia kikamilifu ikafunguliwa kwenye
Makazi hayo

Aidha kwa mujibu wa Mkuu huyo wa Mkoa ili kufikia uzee ulio mwema,uzee
ambao ni wa baraka,uzee wa ushauri,uzee wa kuelekeza unatokana na
mipango mizuri ya serikali na hasa serikali ya awamu ya tano ya Dkt
John Pombe Magufuli.

“Sasa yote hayo yanawezekanaje,yanawezekanaje kufikia uzee wa
baraka,uzee wa ushauri,uzee wa kuelekeza inakuwaje,ni kutokana na
mipango mizuri ya serikali na hasa serikali ya awamu ya tano ya Dkt.
John Pombe Magufuli”alisisitiza Dkt Nchimba.

Tarehe,01 Oktoba,ya kila mwaka ni siku ya Kimataifa ya wazee na mwaka
huu maadhimisho hayo yanafanyika kimkoa huku kauli mbiu ikiwa“Familia
na Jamii Tuwajibike kuwatunza wazee”.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...