wazee busega 1.jpg

“Familia na Jamii Tuwajibike Kuwatunza Wazee”, hii ndiyo kaulimbiu ya kilele cha siku ya Wazee mwaka huu. Maadhimisho ya siku ya Wazee Duniani hufanyika ifikapo tarehe 01 Oktoba kila mwaka. Wilaya ya Busega imeweza kuazimisha siku hiyo kwa kujadili mambo mbalimbali yanayowahusu wazee katika ukumbi wa Silsos, Nyashimo.


Mgeni rasmi katika siku hiyo Wilayani Busega Mhe. Tano Mwera, Mkuu wa Wilaya ya Busega, ameeleza kwamba serikali inajali na kutambua mchango wa wazee nchini hivyo waondoe shaka kuhusu masuala yanayowahusu na kuongeza kwamba serikali ipo bega kwa bega kuhakikisha wazee wanatunzwa na jamii kama kaulimbiu ya mwaka huu isemavyo.


Aidha Mhe. Mwera ameagiza kuwe na utaratibu wa ushiriki wa wazee katika shughuli za maendeleo kwa ngazi ya vijiji kwani wengi wao hawana uwezo, hivyo wasilazimishwe kushiriki katika shughuli za maendeleo. Kwa upande mwingine ametoa angalizo kwamba wazee wasitumie uzee kukwepa ushiriki wao kwenye shughuli za maendeleo, hasa kwa wale wanaojiweza.


Mwakilishi wa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Busega, Dismas Ijagala, amekiri kwamba wazee wana nafasi kubwa katika maendeleo na kwa kupitia mipango mbalimbali ya Kitaifa ikiwemo Mpango wa kunusuru kaya masikini TASAF. Mpango wa TASAF Wilayani Busega una jumla ya kaya lengwa 3,065 na kati ya hizo kaya za wazee zilizopo kwenye mpango ni 822, aliongeza Mratibu wa TASAF Wilaya ya Busega Bi. Wema Mmari.


Awali Mganga Mkuu wa Wilaya Dkt. Godfrey Mbangali amewahakikishia kwamba matibabu ya wazee hayana malipo kama Sera ya Taifa ya Wazee ya Mwaka 2003 inavyoagiza. Pia Dkt. Mbangali alianisha baadhi ya magonjwa yanayowasumbua zaidi wazee ikiwemo magonjwa ya moyo, mifupa, matatizo ya macho na saratani. Tunaendelea kuboresha zaidi huduma za afya kwa wazee. Tumeweza kuanzisha chumba cha wazee kwenye Hospitali yetu ya Wilaya na tunazo dawa asilimia 95.8% kwa magonjwa ya wazee, aliongeza Dkt. Mbangali.


Kwa upande wa Uongozi wa Baraza la Wazee Busega linaishukuru serikali kwa ushirikiano wao na kujali mchango wa wazee katika jamii. Tunaishukuru Ofisi ya Mkurugenzi Mtandaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Busega kwa kushirikiana na kuwa kama mlezi wa Baraza la Wazee Busega kwani hata kodi ya Ofisi yetu inalipwa na Ofisi ya Mkurugenzi, na mambo mengine mengi ikiwemo kutuwezesha baiskeli mbili kwaajili ya Uongozi wa Baraza la Wazee, alisema Katibu wa Baraza la Wazee Busega Ndg. Kapeje Linti.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...