Na Richard Mwaikenda, CCM Blog, Dodoma
BARAZA la Mawaziri limekoma leo kuendelea na shughuli za kikazi mara atakapoapishwa Rais Mteule, Dk. John Magufuli kwenye Uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma .
Taarifa hiyo imetolewa na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbas alipokuwa akizungumza na vyombo vya habari jijini Dodoma jana, kuhusu kukamilika kwa maandalizi ya kuapishwa kwa Rais Mteule, Dk Magufuli.
Dk Abbas alisema kuwa kisheria ni kwamba Baraza la Mawazili la 2015-2020 mwisho wake ni mara tu Rais Mteule atakapoapishwa kushika kipindi chake cha pili cha miaka mitano. Majukumu yote yatafanywa na makatibu wakuu wa wizara hadi atakapotangaza baraza jipya.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...