Shirika lisilo la kiserikali la Gender Action Tanzania (GATA) lililokuwa likijikita katika utazamaji wa Uchaguzi Mkuu uliofanyika hivi karibuni limeishukuru Tume ya Uchaguzi kwa kusimamia Uchaguzi ambao ulikuwa wa haki wenye kufuata utaratibu.

Akizungumza na Wandishi wa habari Jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa Gender Action Tanzania (GATA) Bi.Neema Makando amesema kumekuwa na ushiriki wa wanawake kujitokeza katika kugombea nafasi mbalimbali za siasa kuanzia ngazi ya urais,wabunge mpaka madiwani kwa vyama vyote vya siasa.

"Hii inaonesha kuwa jamii imeanza kubadilika na kuwa na mtazamo chanya kuwa Wanawake wanaweza kuwa katika ngazi za uongozi". Amesema Bi.Neema.

Aidha Bi.Neema amesema wameshuhudia uwepo wa mawakala katika vituo vya kupigia kura licha ya kuwepo kwa machapisho baina ya mawakala na wasimamizi wa uchaguzi kwa baadhi ya vituo wakati wa kuingia kwenye vituo vya kupigia kura.

Pamoja na hayo Bi.Neema amesema kuwa utoaji wa elimu ya Mpiga Kura ulifanyika kwa wingi na kwa njia mbalimbali ikiwa ni pamoja na kutumia vipindi vya rediona runinga, magari ya matangazo, mitandao ya kijamii na kwenye vyombo vya usafiri.

Sambamba na hayo Bi.Neema amesema katika Uchaguzi huo Makundi maalumu yaliwezeshwa kushiriki katika zoezi la kupiga kura hivyo kulikuwa na karatasi maalum za nukta nundu kwa walemavu wasio ona na wanaoweza kutumia nukta nundu.Mkurugenzi Mtendaji wa Gender Action Tanzania (GATA) Bi.Neema Makando akizungumza mbele ya Waandishi wa vyombo vya habari leo jijini Dar,wakieleza taarifa ya awali ya utazamaji wa uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2020 uliofanyika hivi karibuni 

Baadhi ya Wanahabari wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri kwenye mkutano huo 

Mkurugenzi Mtendaji wa Gender Action Tanzania (GATA) Bi.Neema Makando akifafanua jambo kwa Wanahabari namna walivyoweza kufanya kazi yao ya utazamaji katika Uchaguzi Mkuu 2020 uliofanyika hivi karibuni nchini.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...